Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Faustina Kowalska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Helena Kowalska ujanani.
Sista Maria Faustina waSakramenti Kuu mwaka1938, kidogo kabla ya kufa.

Maria Faustina Kowalska (kabla hajaingiautawani aliitwaHelena Kowalska; anafahamika zaidi kamaMtakatifu Faustina;Głogowiec (soma Gwogoviec) karibu yaŁódź (soma Wodz) nchiniPolandi,25 Agosti1905 -Kraków,Polandi,5 Oktoba1938[1]) alikuwabikira anayejulikana hasa kamamtume wafumbo laHuruma ya Mungu,katibu waYesu Mwenye Huruma namwandishi waHafidhi[2].

Anaheshimiwa kamamtakatifu waKanisa Katoliki, kutokana na sifa zake kamamtawa waShirika la Bibi Yetu wa Huruma,mcha Mungu, aliyejaliwanjozi namadonda ya Yesu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe yakifo chake[3].

Maisha

Helena Kowalska alizaliwa tarehe25 Agosti1905, kama mtoto wa tatu baina ya watoto kumi wa Stanisław na Marianna Kowalski, wakulima kutoka kijiji kinachoitwaGłogowiec; wote wawili walikuwamaskini lakini waadilifu.

Tangu alipokuwa na umri wa miaka saba alisikiawito wa maisha ya utawa. Mwaka1916 alianzashule ya msingi kijijiniŚwinice Warckie (soma Shvinitse Vartskie).

Baada ya miaka mitatu ya mafunzo, licha ya matokeo yake mazuri alilazimika kumalizaelimu yake na kuanza kufanyakazi kwa watu tajiri kamamtumishi wa ndani nyumbani namlezi wa watoto[4].

Alipokuwa na umri wa miaka 17 aliwaambia wazazi wake kuwa alitaka kujiunga na utawa. Wazazi wake hawakutaka kumpotezabinti yao mpendwa, kwa hivyo walimkatalia katakata mara mbili ombi lake.

Mnamo mwaka1922 alikwendaŁódź kufanya kazi ya mtumishi wa ndani[5].

Mwaka1924, wakati wa kuchezangoma katika hifadhi ya "Venice" mjini Łódź alikuwa na maono ya "Yesu aliyeteswa sana, kavuliwa nguo, na mwili wake wote umejaa vidonda na anaguna, akisema maneno haya kwangu:Kwa muda gani nitakuvumilia mpaka utakubali?" (Hafidhi 9)[6].

Bila kuwajulisha wazazi wake alipandagari la moshi akaendaWarszawa (soma Varshava). Baada ya kufika mjini huko alielekeakanisa la kwanza lililoko karibuni yaani Kanisa la Mtakatifu Yakobo katikabarabara Grójecka.

Akakaa kijijiniOstrówek (soma Ostuvek), ambapo hadi mwaka1925 alifanya kazi kwa akina Lipszyc. Hakuchoka kutafutashirika la kitawa ambalo limpokee. Mara nyingi alikataliwa lakini hakukata tamaa kutafuta.

Hatimaye Sista Michael Moraczewska, mkuu wa Shirika la Bibi Yetu wa Huruma mjini Warszawa, alionyesha nia ya kumpokea shirikani mwao, ikiwa Helena ataweza kuchangia kiasi kidogo chafedha (kamamahari) cha kununua mavazi ya kitawa[7].

Tarehe1 Agosti1925 alijiungaShirika la Bibi Yetu wa Huruma mjiniWarszawa barabara ya Żytnia na kuanzaupostulanti.

Mazoezi ya kiroho namafungo mengi vilimchosha Helena. Kwa sababu hiyo alishinda wiki chache mjini Skolimów (soma Skolimuv) karibu na Warszawa, akiwa na nia ya kusaidiaafya yake, kutiamwili wake nguvu.

Tarehe23 Januari1926 alikwendaKraków.

Tarehe30 Aprili1926 Helena alianzaunovisi na wakati huo alipewa jina la Maria Faustina.

Tarehe 30 Aprili1928, huko Kraków, aliwekanadhiri za kwanza: yausafi wa moyo,umaskini nautiifu.

Akiwa sista mdogo wa nadhiri za kwanza (kipindi kinachodumu miaka mitano ambapo kila mwaka alirudianadhiri) sista Faustina alifanya hasa kazi yaupishi katikanyumba nyingi za shirika. Alikaa katika nyumba ambayo ilikuwa pembeni mwa barabara iliyoitwa Żytnia, mjini Warszawa[8] na baadaye aliishiVilnius, mji mkuu waLithuania (ambao wakati huo ulikuwa upande wa nchi ya Polandi), tena mjini Warszawa, katikamonasteri karibu na barabara ya Hetman na mjini Płock ambapo alikaa zaidi ya miaka miwili. Katika mji huo wa mwisho alifanya kazi ya mwuzaji katika duka la mikate.

Tarehe1 Desemba1931 Faustina alianza muda wake wa majaribio ya tatu katika maisha ya utawa mjini Warszawa. Wakati huo, baba Edmund Elter waShirika la Wajesuiti,profesa wamaadili, [[mafunzo ya kuhubiri] (hotuba), nabalagha katikaChuo Kikuu cha Gregoriana mjiniRoma, alimhakikishia kwamba yuko katika njia ya hakika na nzuri, na uhusiano wake na Yesu si wa mzaha, wala si wa mauzauza au mazingaombwe.

Mnamo tarehe1 Mei1933, Faustina aliwekanadhiri za milele mjini Kraków (soma Krakov).

Baada ya nadhiri alitumwa mji wa Wilno (soma Vilno). Alikuwa huko hadi mwaka1936, akishughulika na kazi ya kutunzabustani. Hapo ndipo alikutana na BabaMichał Sopoćko (soma Mihaw Sopochko), ambaye atakuwamuungamishi wake na Baba wa kiroho (kwa sasa niMwenye Heri waKanisa Katoliki), Yesu alimwambia "Huyu ndiye mtumishi wangu mwaminifu, yeye atakusaidia kutimiza mapenzi yangu hapa duniani”(Hafidhi 263).[9]

Baada ya ugunduzi waugonjwa wakifua kikuu (TB) mnamo 1936[10], sista Faustina alisafiri kwenda mji wa Kraków, njiani alisimama katika kijiji chaWalendów naDerdy (soma Valenduf na Derdi) kwa muda wa majuma machache.

Alipowasili mjini Kraków alishinda zaidi ya miezi minane katikahospitali yaPrądnik (soma Pradnik). Alitibiwa pia katika nyumba ya shirika mjini RabkaRabka (soma Rabka).

Alifariki mnamo tarehe5 Oktoba1938[11] katika nyumba ya shirika katika mtaaKraków-Łagiewniki (soma Krakuv - Wagievniki)[12][13].

Heshima baada ya kufa

Mazishi ya Sista Faustina yalifanyika tarehe7 Oktoba 1938[14]. Alizikwa katikashamba la Mungu la Shirika huko Łagiewniki.

Tarehe25 Novemba1966 mabakaa yake yamezikwa tena mahali pengine yaani kakika kanisa dogo la shirika (na tangu mwaka1968 kanisa hilo liliwekwa katika orodha ya mahalipatakatifu katikajimbo kuu la Kraków). Sasa hivi masalia ya mwili wake yamo ndani yajeneza la jiwe, katikaaltare, chini yapicha "Yesu, ninakutumainia" ambayo inajulikana kwafadhili na ilichorwa naAdolf Hyła (soma Adolf Hywa).

Tarehe18 Aprili1993, ambapo Sista Faustina alitangazwa naPapa Yohane Paulo II kuwamwenye heri, masalia yake yaliwekwa hadharani.

Kanisa Katoliki linamheshimu kama tangu alipotangazwa naPapa huyohuyo kuwamtakatifu tarehe30 Aprili2000.

Ufunuo na uzoefu wa uhusiano maalumu baina yake na Mungu

Kutokana na agizo la Baba Michał Sopoćko, halafu pia la baba Yusufu AndraszSJ (muungamishi wa Kraków), Sista Faustina alikuwa anaorodhesha maono yake yote yaliyo mengi mengi namafunuo: yote yalichapishwa baadaye katikaHafidhi (Diary).

Matokeo haya yote hayakuhusu maisha yake ya kiroho tu (kwa mfano uhusiano baina yake naYesu,malaika na watakatifu), lakini zaidi ya hiyo misheni yake ya kinabii, ambayoKristo alimjalia Faustina kwa ajili ya kumtumia duniani.

Ujumbe wake wahuruma unafanana naukweli waBiblia juu yaupendo wa huruma wa Mungu ambayo huletwa naye kwa kilabinadamu na pia ulikuwawito kwa kutangaza ukweli huo kwa nguvu mpya na ushahidi wa maisha, matendo, maneno nasala.

Tukio hilo lilisaidiwa na njia mpya za ibada alizopewa na Yesu,picha "Yesu, ninakutumainia", uanzishaji waSikukuu ya Huruma ya Mungu, sala yaRozari ya Huruma ya Mungu, sala kwa ajili yakifo chakemsalabani (Saa ya Huruma) na tendo la kueneza ibada ya Huruma ya Mungu.

Yesu alitoa ahadi kubwa kwa wale watakaotekeleza maombi haya kwaimani kubwa kwa Mungu na kufanya matakwa yake na kuwapendajirani zao kamanafsi zao.

Kutokana na maandiko yake Huruma ni kubwa kuliko sifa nyingine za Mungu ambazo binadamu anazishuhudia. Hiyo haina mipaka wala kikomo na inapatikana kwa binadamu wote, hasa kwa watu wakosefu. Kristo alipendekeza kuwa na imani kamili kwa huruma yake Mungu na aliomba watu wawatimizie wenzaomatendo ya huruma kutokana na mapenzi yake.

Kwa mujibu wa "Hafidhi", tarehe22 Februari1931, alipokuwa mjiniPłock Sista Faustina alikuwa na maono ya Yesu akiwa amevaakanzu nyeupe. Aliinuamkono wake wa kulia kwaishara ya kutoabaraka, mkono wake wa kushoto uligusa mavazikifuani katika mahali ambapo makengee mawili yalimulika. Mojawapo lilikuwa narangi nyekundu huku lingine nyeupe (lilizingia). Hapo ndipo aliposikia: "Chora picha kulingana na muundo unaouona yenye maandiko ‘Yesu, ninakutumainia’. Napenda picha hii itukuzwe, kwanza kwenye kikanisa chenu, na badadaye duniani kote. Ninaahidi kwamba roho itakayotukuza picha hii haitaangamia. Mimi pia ninaahidiushindi juu ya maadui na hasa katika saa ya kufa. Mimi mwenyewe nitaikinga kamautukufu wangu mwenyewe. "(Hafidhi 47-48)[15]. Njozi hii ilianzisha kazi yake ya kinabii.

Maono yake mengine yalihusu uanzishaji waSikukuu ya Huruma ya Mungu, ambayo watu waiadhimishe Jumapili ya kwanza baada yaPasaka. "Natamani iwepo Sikukuu ya Huruma. Ninapenda picha ile utakayoichora na brashi; kuwa waweka heri juu yake Jumapili ya kwanza baada ya Pasaka, na Jumapili hii iwe Sikukuu ya Huruma. Nataka mapadri watangaze hii Huruma Yangu kubwa kwa roho za wenyedhambi. "(Hafidhi 49-50)[16]. Mwezi Novemba1932, wakati wa uungamaji wa mafungo ya kiroho ya padre Edmund Elter SJ, Faustina alipata ushahidi wake wa kwanza uliothibitisha kwamba maono yake yalikuwa na asili yaufunuo.

Picha ya Yesu mwenye Huruma imechorwa naEugeniusz Kazimirowski mjini Vilnius. Mchoraji huyo alimaliza kazi hiyo mwezi Juni1934. Kwa mujibu wa mtakatifu,taswira hiyo haikujaa nauzuri ambao hujaza kilakiumbe kinachojitokeza kwenye maono. "Si kwa uzuri wa rangi, wala wa brashi kulalapo ukuu wa picha hii, lakini katika neema yangu. "(Hafidhi 313) - Yesu alimjibu.[17]

Tarehe9 Juni1935 Faustina alisikia maneno haya: "Na kwa maombi yako, wewe na wenzako mtapatarehema kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili yadunia"(Hafidhi 435)[18]. Yesu alisema kwamba Mungu apenda kuwe na shirika ambalo litatangaza Huruma ya Mungu kwaulimwengu na kwa sala zake kuipata Huruma kwa ajili ya dunia (Hafidhi 436).[19] Katika mafunuo ya baadaye alieleza kuwa haitakuwa shirika moja, lakini kazi kubwa katika Kanisa, ambayo itajumuisha mashirika ya kutafakari na ya kitume, na waumini wote duniani kote.

Mnamo tarehe 13 -14 Septemba1935 Yesu alimtajia maneno ya sala inayojulikana kamaRozari ya Huruma. Kwa mujibu wa hafidhi yake mtakatifu Faustina, Yesu aliwaahidia wote wanaosalidua hiyo kwa imani kwamba wao watajaliwaneema zake zote, hasa neema yakifo chema chenye shwari na hiyo itawahusu hata wao ambao wakifa wataoombewa sala hiyo na watu wengine.

Mnamo Oktoba1937 Yesu alimdokezea Sista Faustina namna mpya ya ibada ya Huruma ya Mungu, yaani aliamuru watu waheshimu muda wa kifo chake msalabani:"Saa tisa alasiri, omba Huruma yangu, hasa kwa ajili ya wakosefu; na walau kwa kitambo kifupi jizamishe kwenye Mateso yangu, hasa pale nilipoachwa peke yangu bustanini katika saa ya masikitiko makuu. Hii ni saa ya huruma kubwa kwa dunia nzima." (Hafidhi. 1320).[20]

Hafidhi

Hafidhi yake Sista Faustina imeandikwa mjini Vilnius na Krakow kati ya 1934 na 1938 kwa msingi wa maelekezo ya Yesu, "Andika chini maneno haya, ambia ulimwengu juu ya rehema yangu na upendo wangu. Moto wa huruma unanichoma. Nataka kuumwaga nje kwa ajili ya nafsi ya binadamu. Oh, maumivu gani wananisababishia kwangu wakati hawataki kukubali wao ! Fanya lolote lililo kwenye uwezo wako ili kueneza ibada kwa rehema yangu. Mimi nitatimiza kile mkosacho. Mwambie mwanadamu aumwaye kwamba asogelee na Moyo Wangu wa huruma, nami nitamjaza na amani. Mwambie [watu wote], binti yangu, ya kwamba mimi ni Upendo na Huruma yenyewe". (Hafidhi 1074)[21]), na agizo la waungamishi: Pd. Michael Sopocko na Baba Joseph Andrasz SJ na kwa idhini ya wakuu wa Usharika. Sentensi za kwanza ambazo zimehifadhika zimeandikwa Julai 1934.Sura za awali kabisa wamechomwa moto na mwandishi, ambaye hivyo alitimiza agizo la malaika wa tuhuma. Kwa sababu hii hafidhi ina maumbile yake ya mwisho yenye mlolongo wa fujo kidogo. Maingizo yake ya mwisho yamefanywa mnamo Juni mwaka 1938. Kwa jumla hafidhi ina sehemu sita.„Hafidhi" ni maelezo ya maisha ya mwandishi rohoni mwake. Anasimulia juu ya maisha yake ya kila siku rohoni na uzoefu wake wa uhusiano maalumu baina yake na Mungu, kwa mfano maono ya Kristo, Mama wa Mungu, malaika na watakatifu, maono ya jahanamu, toharani na mbinguni... Yesu Kristo anapendekeza Huruma ya Mungu kama wokovu wa pekee kwa dunia nzima (Watu hawatakuwa na amani mpaka zamu igeuke na uaminifu kwa huruma Yangu (Hafidhi 300))[22]

Hafidhi inashirikisha pia hotuba ya Huruma ya Mungu ambayo Yesu Kristo alimletea mhusika wetu mtakatifu pamoja na pendekezo la aina jipya za ibada. Hafidhi ya Faustina Mtakatifu inaelezea upendo wake wa Utatu Mtakatifu, ambao ulimwunganisha na Mungu. Kutokana na kumbukumbu inaelekea kwamba tendo la kutangaza Huruma ya Mungu limekuwa kiini kikuu cha maisha yake Maria Faustina.Katika Hafidhi tunapata pia maelezo ya neema za ajabu, baraka ya Mungu lakini pia matatizo na mateso ambayo yeye alilazimika kuyakabili, wajibu wake, maana yake maalumu, ushahidi wa utakatifu wake na thawabu kwa maisha yake mazuriUtaiandaa dunia kwa ajili ya kuja kwangu mara ya mwisho (Hafidhi 429)[23].Kisha nikasikia maneno, Wewe ni shahidi wa Huruma yangu. Wewe utasimama mbele ya kiti changu cha enzi milele kama ushahidi hai kwa Huruma Yangu (Hafidhi 417)[24].Mnamo Machi 1959 kutokana na tafsiri kosefu ya Hafidhi, Ikulu Takatifu ilitoa amri iliyokataza watu wasieneze ibada ya Huruma ya Mungu kwa namna yake Sista Faustina (AAS 6 Machi 1959, u. 271). Licha ya tukio hilo kutokana na juhudi zake Askofu Karol Wojtyła (baadaye Papa Yohane Paulo II) taratibu ya kumpatia Faustina hali ya mtu mwenye heri ilianza mjini Kraków. Marufuku haijafutwa mpaka mwaka 1978. Toleo la kwanza la kumbukumbu zake za kiroho lilitolewa mnamo 1981.Kitabu kimekuwa kinatafsiriwa kwa lugha nyingi. Akiongozwa na hafidhi zake Faustina, Papa Yohane Paulo II aliandika Ensiklika yake “Dives in misericordia” (1980) juu ya Mungu “aliye na huruma mno”Kiini cha maabudu haya ni kujenga ule uaminifu kwa Mungu ambao unatimizwa kwa namna ya kutekeleza dhamira zake zilizoko kwenye amri zake, wajibu wa jukumu yake, ualimu wa Injili na ilhamu za Roho Mtakatifu zinazojulikana. Nguzo ya pili ya Maabudu haya ni mwenendo wa kuwahurumia binadamu kwa njia ya matendo, maneno na sala.

Mchakato wa kumpatia hadhi ya mtu mwenye heri na baadaye pia hadhi ya mtu mtakatifu

Terehe 5, Aprili 1978, kufuata ombi la Kardinali Karol Wojtyła, Ikulu Takatifu ilibatili ibada ya Huruma ya Mungu kwa namna zilizochipukiza kutoka Maono ya Sista Faustina.Tarehe 7, Machi 1992 Yohane Paulo II alitoa azimio yake Faustina Kowalska, tena tarehe 21, Disemba 1992 – akatoa azimio la muujiza uliotokana na maombezi wake. Mnamo 18, Aprili 1993 lilitokea tukio Faustina mwenye heri ambalo liliongozwa na Papa Yohane Paulo II. Kaama muujiza unaohitajika kwa ajili ya kumwinua mtu altareni lilichukuliwa tukio ambapo mwanamke aliyekuwa ameshambuliwa na maradhi ya Lymphedema alipona (Lymphedema (kiingereza),Lymphedema (kifaransa)). Tarehe 30, Aprili 2000 uliwadia wakati kwa kumtangaza Faustina mtakatifu, na tukio hili liliongozwa na Papa Yohane Paulo II pia. Sherehe zilifanyika mijini Roma na Kraków. Hapo ndipo sikukuu ya Huruma ya Mungu ilianzishwa Kanisa nzima. Kama muujiza, lilichukuliwa tukio la kumponya padre Mpolandi ventrikali yake ya upande wa kushoto ambayo ilikuwa imeharibiwa (http://sw.wikipedia.org/wiki/Moyo#). Mnamo tarehe 10, Desemba 2005 kutokana na amri ya Askofu Mkuu Władysław Ziółek, alitangazwa mlinzi mtakatifu wa mji wa Łódź.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Alan Butler and Paul Burns, 2005,Butler's Lives of the Saints, Burns and OatsISBN 0860123839 page 251
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/73200
  3. Martyrologium Romanum
  4. s. M. Elżbieta Siepak, ZMBM,Dar Boga dla naszych czasów, [on-line]. faustyna.pl.
  5. Franciszek Cegiełka,Siostra Faustyna Szafarka Miłosierdzia Bożego, Londyn-Warszawa, Michalineum, 2003, pp. 15-18.ISBN 83-7019-245-9
  6. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 8.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  7. Franciszek Cegiełka,Siostra Faustyna Szafarka Miłosierdzia Bożego, Londyn-Warszawa,Michalineum, 2003, pp. 23-29.ISBN 83-7019-245-9
  8. Franciszek Cegiełka,Siostra Faustyna Szafarka Miłosierdzia Bożego., Londyn-Warszawa, Michalineum, 2003, pp. 37-43.ISBN 83-7019-245-9
  9. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 113.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  10. M. Elżbieta Siepak ZMBM ,Dar Boga dla naszych czasów. [on-line]. www.faustyna.pl.(Kipolandi)
  11. Franciszek Cegiełka,Siostra Faustyna Szafarka Miłosierdzia Bożego., Londyn-Warszawa, Michalineum, 2003, pp. 229-235.ISBN 83-7019-245-9
  12. "Kalendarium. www.faustina.pl (Kipolandi)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2012-05-04. Iliwekwa mnamo2012-07-22.
  13. Kalendarium. www.faustyna.pl. (Kipolandi)
  14. Kalendarium. www.faustyna.pl. (Kipolandi)
  15. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 37.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  16. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 37.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  17. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 125.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  18. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 161.,ISBN 83-7502-0 12-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  19. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 162.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  20. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 375.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  21. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 322.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul)
  22. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 122.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul
  23. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 160.,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul
  24. Faustyna Kowalska,Dzienniczek. Miłosierdzie Boże w duszy mojej., Warszawa, 2001, p. 156,ISBN 83-7502-012-5 (Diary.Divine Mercy in My Soul

Marejeo ya Kiswahili

  • Pd. Leandry Kimario,O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 301-302

Viungo vya nje

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Faustina_Kowalska&oldid=1465545"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp