Familia (kutokaKilatini "familia") ni kikundi chawatu wanaokaa pamoja kamababa,mama nawatoto. Kikundi hicho mara yingi ni sehemu yakundi kubwa zaidi laukoo unaounganisha watu wenye asili katikauzazi wa pamoja.
Katika nchi nyingi zaAfrika familia ndogo ya baba, mama na watoto kwa kawaida ni sehemu tu ya familia kubwa zaidi pamoja nandugu wa baba na mama, akinababu nabibi na kadhalika. Lakini hata Afrika kuna taratibu tofautitofauti kama ni ndugu wa baba au ndugu wa mama wanaotazamiwa kuwa karibu zaidi kwa watoto wa familia ndogo.
Vilevile kuna tofauti kamamuundo wa kawaida nimume mmoja na wake wengi na kila mmoja akiwa na watoto wake tena.
Katika jamii za nchi zilizopita kwenyemapinduzi ya viwandani kamaUlaya naMarekani familia inamaanisha hasa familia ndogo inayokaa pamoja katikanyumba. Ukoo haujapotea lakini umuhimu wake umepungua sana na mara nyingi ni chaguo la watu ndani ya ukoo kama wanapenda kujumuiana na ndugu zao au la.
Katikamazingira yamiji mikubwa au pale ambako koo za kale zimeporomoka na kuachana kunajumuiya ndogo sana kama mama na watoto ambao ni familia bila baba auwanaume. Aina hii ya familia yenyemzazi mmoja tu imepatikana pia kama familia ya baba na watoto kama utamaduni unamruhusu baba peke yake kulea watoto.
Katika mazingira yaumaskini,vita au mabadiliko ya haraka sana kuna pia watoto wengi wanaoishi kwa bibi au babu na hata hali hii ni aina ya familia.
Families Australia – independent peak not-for-profit organisation. familiesaustralia.org.au
FamilyPlatform – A consortium of 12 organisations providing input into the European Union's Socio-Economic and Humanities Research Agenda on Family Research and Family Policies.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuFamilia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.