Eneo la EurasiaNamna mbalimbali za kuchora mpaka kati ya Ulaya na Asia.
Eurasia nijina linalotumika kutaja kwa pamoja nchi zote zaAsia naUlaya. Jina hilo linaunganisha maneno "Europa" na "Asia".
Hali halisimabara ya Ulaya na Asia yako pamoja kama nchi kavu mfululizo na hakunabahari inayoyatenganisha. Kwa hiyo Ulaya na Asia haziitwi mabara kwa sababu zakijiografia bali kwa sababu zakihistoria na zakiutamaduni tu.
Desturi hii inatokana naWagiriki wa Kale waliokuwa watu wa kwanza wa kugawadunia katika sehemutatu tofauti (Ulaya, Asia naAfrika) na hivyo kuweka msingi wa ugawaji wa dunia kwa mabara.
Wataalamu wengi wa jiografia wanaona ya kwambamasi ya nchi kavu inayojumlisha Ulaya na Asia inatabia zote zabara moja na hivyo hutumia jina la "Eurasia". Karibu eneo lote liko juu yabamba la gandunia lilelile, yaaniBamba la Ulaya-Asia.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.