Etimolojia(kutokagir. ἐτυμολογία etimología, kupitiaing. etymology) ni elimu ya maana ya maneno na asili zao.
Maneno pamoja na matamshi natahajia hubadilika polepole. Yanaweza kuunganishwa au kufupishwa. Maneno huhamia kutoka lugha moja hadi nyingine na hapo yanaweza kubadilisha maana. Maneno mapya yanabuniwa kwa vitu vipya visivyojulikana awali.
Kiswahili nilugha ya Kibantu na hapo asili ya maneno mengi inaweza kutambuliwa kwa kulinganisha lugha mbalimbali ya Kibantu. Lakini Kiswahili ni pia lugha iliyopokea maneno mengi kutoka nje, hasa kutokaKiarabu, baadaye kutokaKireno na lugha zaKihindi na siku hizi kutokaKiingereza. Ilhali lugha hizi zimepokea pia maneno kutoka asili nyingine wakati mwingine historia ya neno ni kama safari katika historia ya kibinadamu.
"Etimolojia" imefika katika Kiswahili kutoka Kiingerezaetymology lakini kiasili ni neno la Kigiriki cha Kale lililoundwa kuotokana maneno ya ἔτυμονetimon ("maana ya kweli") na -λογία-logia ("somo la..", "elimu kuhusu"). Neno hili la Kigiriki lilipokelewa katika Kilatini ambacho baadaye kilikuwa lugha ya elimu katika Ulaya ya MAgharibi wa karne nyingi na hivyo kuingia katika lugha nyingi za Ulaya.[1]
Kitabu ina asili yaKiarabu( كتاب, kitabun); inaonekana ni wafanyabiashara Waislamu waliotumia lugha ya Kiarabu waliopeleka kitu hiki katika mazingira yasiokuwa na maandishi kwa hiyo neno la kigeni likapokelewa moja kwa moja kwa kitu kigeni.
Samaki pia ni neno lenye asili ya Kiarabu(سمك samakun); bila shaka wenyeji wa Uswahilini walikuwa na neno la Kibantu kwa samaki na hapa kuna swali kwa nini waliaacha neno lao la kiasili kwa neno la nje; kuna hoja ya kwamba kule pwani samaki zilikuwa vyakula vilivyouzwa na wenyeji kwa wageni waliofika kwa jahazi na hivyo waliona faida wakitumia lugha ya wateja.
Muhindi kama jina la nafaka linatunza uhusiano na Uhindi ingawa uwzekano mkubwa ni imefika Afrika kutoka Amerika kupitia Wareno na Wahispania. Katika lugha za Ulaya mara nyingi iliitwa "nafaka ya Uhindi" (ing. Indian corn,far. ble de Inde) kwa sababuKolumbus aliamini ya kwamba alifika Uhindini ya Asia na Wahispania pamoja na Wareno waliita nchi walizotawala katika Amerika "India" kwa karne zilizofuata. Hata hivyo kuna uwezekano ya kwamba nafaka hii ilifika pia kutoka Bara Hindi moja kwa moja kwa sababu kuna uwezekano ya kwamba ilijulikana pale kabla ya Kolumbus[2][3]. Inawezekana pia ya kwamba wenyeji wa pwani walitunga jina hilikwa kudokeza ni nafaka kutoka sehemu za mbali.[4][5]
Maneno kamaTanzania,UKIMWI auBAKITA yametungwa juzijuzi tu kwa unganisha sillabi ya majina mengine:TANganyika naZANzibar kuwa Tanzania,Uhaba waKIngaMWIlini kuwa Ukimwi,BAraza yaKIswahiliTAnzania kuwa Bakita.
Kamusi ya Kiswahili - Kifaransa iliyotolewa na Charles Sacleux mwaka 1939 hadi sasa ina maelezo bora na pana ya etimolojia ya maneno ya Kiswahili - lakini inatoa maana kwa Kifaransa tu.
↑Vivyo hivyo makala hii kwenye tovuti ya M. Kumar and J. K. S. Sachan kwenye tovuti ya Rajendra Agricultural University[1]Ilihifadhiwa 30 Aprili 2011 kwenyeWayback Machine.
↑Kuna mifano ya etimolojia ya aina hii kwa muhindi katika nchi za Ulaya: katika Ujerumani ya Kusini, Austria na Slovenia muhindi iliitwa "nafaka ya Kituruki" ("türk" au "Türkisch Weizen") ingawa haitokei kule, lakini jina limetokea kwa kutaja asili ya nchi ya mbali.