Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Eswatini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufalme wa Eswatini
Umbuso weSwatini (Kiswazi)
Kingdom of Eswatini (Kiingereza)
Kaulimbiu:Siyinqaba (Kiswazi)
"Sisi ni ngome"
Wimbo wa taifa:
Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati
"Mungu, Mpaji wa Baraka kwa Waswati"
Mahali pa EswatiniMahali pa Eswatini
Ramani ya EswatiniRamani ya Eswatini
Miji mikuuMbabane (serikali)
Lobamba (bunge)
Mji mkubwaMbabane
26°19 S 31°08 E
Lugha rasmiKiswati
Kiingereza
Kabila84Waswati
10Wazulu
6 wengine

Eswatini (jina rasmi:Ufalme wa Eswatini, piaUswazi) ni nchi ndogo isiyo na pwaniKusini mwa Afrika. Imepakana naAfrika Kusini pande zote isipokuwa kaskazini mashariki inapopakana naMsumbiji. Mnamo 2023, Eswatini ilikuwa na idadi ya watu takriban milioni 1.2 na kuwa nchi ya 155 duniani kwa idadi ya watu.Miji mikuu niMbabane naLobamba huku Mbabane ukiwa pia mji mkubwa nchini humo.Kiingereza naKiswazi ndizolugha rasmi.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwawawindaji wa jamii yaWasani.

Katikakarne za kwanzaBK walifika wahamiajiWabantu wenyeujuzi wakilimo nauhunzi.

Waswati walianzishaufalme wao katikati yakarne ya 18 chini yaNgwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka1881.

Baada yavita kati yaWaingereza naMakaburu, Swaziland ilukuwanchi lindwa yaUingereza tangu mwaka1903 hadi1967.

Chini yamfalmeSobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana (1921-1982), Swaziland ilipatauhurutarehe6 Septemba1968.

Siasa

[hariri |hariri chanzo]

Eswatini inatawaliwa tangu mwaka1986 namfalmeMswati III. Mfalme anapingwa mara nyingi kwa sababu anatumiapesa nyingi kwa ajili yake binafsi ilhali wananchi nimaskini sana. Kwa muda mwingi wauhuru wa nchikatiba imesimamishwa, na mfalme ametawala peke yake.

Watu

[hariri |hariri chanzo]
Mwanamke kutoka Eswatini akicheza.

Wakazi wengi ni wakabila laWaswati na kuongealugha yaKiswati ambacho nilugha rasmi pamoja naKiingereza. Shuleni kinafundishwa piaKireno.

Upande wadini, 89.3% niWakristo wamadhehebu mbalimbali, hasaWaprotestanti, lakini piaWakatoliki (5%). Wanaoendelea kufuatadini asilia za Kiafrika ni 0.5% naWaislamu ni 1%.

Afya

[hariri |hariri chanzo]

Eswatini ni kati ya nchiduniani zilizoathiriwa zaidi naUkimwi;umri wawastani unafikia miaka 22 pekee kwa sababu yavifo vingi (64%) vinavyotokana naugonjwa huo uliopata 26% ya watu wazima wote.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]

    Tazama pia

    [hariri |hariri chanzo]

    Viungo vya nje

    [hariri |hariri chanzo]
    WikiMedia Commons
    WikiMedia Commons
    Wikimedia Commons ina media kuhusu:


    Nchi zaAfrikaBara la Afrika
    Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
    Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
    Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
    Nchi wanachama waUmoja wa Afrika (AU)
    Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
    Je unajua kitu kuhusuEswatini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
    Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
    Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Eswatini&oldid=1455560"
    Jamii:
    Jamii iliofichwa:

    [8]ページ先頭

    ©2009-2026 Movatter.jp