- Tazama pia:Eneo la ng'ambo la Ufaransa
Ufaransa ilikuwa na makoloni mengi kote duniani. Hadi leo kuna maeneo yaliyo mbali na Ulaya lakini ama yamekuwa sehemu kamili za nchi hiyo au zinasimamiwa kama maeneo tegemezi yaliyopewa hadhi ya “jumuiya ya ng’ambo ya bahari” (collectivite d’outre mer) katikakatiba ya Ufaransa ya mwaka 2003.
Maaeneo yote yana wawakilishi katika bunge la Ufaransa na pia katikaBunge la Ulaya. Katika Bunge la Ulaya kuna wawakilishi watatu, mmoja-mmoja kwa maeneo katika Atlantiki, Pasifiki na Bahari Hindi.
Jumuiya hizo zilianzishwa kwa mabadiliko ya katiba ya Ufaransa mwaka 2003. Kila jumuiya imeundwa kwa sheria ya pekee.
- Kaledonia Mpya (katikaPasifiki ya kusini) ni eneo la pekee; wakazi walijadili uhuru lakini waliamua kwa kura ya mwaka 2018 kubaki kama jumuiya chini ya Ufaransa.
Ufaransa hutawala au kudai utawala juu ya visiwa vidogovidogo bila wakazi:
Visiwa vya kusini na eneo la Antaktiki (Terres australes et antarctiques françaises)
[hariri |hariri chanzo]Maeneo hayo yanatawaliwa kutoka Réunion. Hakuna wakazi wa kudumu, hivyo ni maeneo ya pekee yasiyo na haki za kisiasa: kuna visiwa vya Amsterdam, Saint-Paul, Crozet, Kerguelen na eneo la Adélieland kwenye Antaktiki, halafu Îles Éparses.