Ukubwa wa eneo linapimwa kwa kuulinganisha na miraba maalumu. Katika mfumo wavipimo sanifu vya kimataifa kizio sanifu nimita ya mraba (inayofupishwa kwa m²). Umbo kama mviringo mwenye eneo la 3m² una eneo sawa na miraba mitatu ya aina hii.
Makadirio ya eneo yana faida nyingi katika maisha ya kila siku. Nikitaka kupiga rangi kuta za chumba naweza kupima maeneo yote ya kuta zake. Kwa mfano chumba cha mita 3x4 na kimo cha mita 2 lina eneo la kuta zake za 28 m² (Kuta 2 zenye upana wa mita 3 x kimo mita 2 ni 2x3=6 x kimo 2 = 12m²; kuta 2 zenye upana wa mita 4 ni 2x4= 8 x kimo 2= 16 m²; 16m²+18m² = 28 m²). Nikijua hii naweza kuuliza dukani je wana rangi gani kwa ajili ya ukuta na kopo la rangi linatosha kwa mita za mraba ngapi? Wakisema 10 m ² najua nitahitaji kununua kopo 3. Katika mfano wa juu naweza kutoa eneo la mlango na madirisha labda zinatosha kopo 2 kubwa na 1 ndogo.
Vivyo hivyo naweza kukadiria kiasi cha mbolea kwa eneo la shamba na kadhalika.