Madini hupangwa katika vikundi maalum kulingana nakemikali ndani yake, au kulingana na muundo zafuwele ndani yake.
Uchunguzi wa madini unaleta habari nyingi kuhusu miamba nahistoria yaDunia.Elimu hiyo inasaidia pia kuelewa nafasi kwa matumizi ya madini tofauti, na kuongozautafiti kwa kupata madini mbadala au kutengeneza madini kwenyemaabara kwa matumizi katikateknolojia.
Wakati mwingine sura auumbo la madini vinaonyesha jinsi yalivyoundwa. Kwa mfano, madini katikamiamba ya mgando(igneous rock) yanasaidia kujuaumri wa mwamba tangu kuganda (kubadilika kutokalava kuwa mwamba). Madini makubwa yanamaanisha mwamba uliopozwa polepole (labda chini yaardhi). Madini madogo humaanisha kuwa mwamba ulipozwa haraka (labda juu ya ardhi, kama kutokavolkeno). Aina za madini katika mwamba pia zinaweza kuonyesha ni mwamba wa aina gani, au kile kilichotokea kwa mwamba tangu kuundwa. Miamba mingi hupewajina kulingana na aina ya madini iliyonayo.
Wataalamu wa elimu madini huangalia madini katika miamba kwa kutumialenzi zamkononi, na kwa undani zaidi wakikata mabapa membamba na kuyachungulia chini yahadubini. Huangalia umbo na ukubwa wa fuwele, narangi ya madini. Maelezo hayo yanasaidia kujua ni madini gani yanayoangaliwa.
Madini hutumika katika mambo mengi tofauti, kama mapambo yavito,kilimo,ufinyanzi, kutengeneza metali na mengine.
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuElimu madini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.