Mji huu mdogo una historia ndefu. Ilitajwa mara za kwanza katika hati ya mwaka994BK.
Katika karne ya 12 ulikuwa mji mkuu wa dola dogo la makabaila wa Mansfeld. Dola hili pamoja na mji wa Eisleben lilitajirika katika karne ya 13 baada ya kugunduliwa matapo yashaba na kuanzishwa kwa migodi ya kuchimba madini haya na tasnia ya kuyeyusha shaba hapa.
Katika karne ya 18 eneo la Mansfeld ilikuwa sehemu ya milki yaSaksonia na baadaye yaPrussia. Baada ya ugawaji wa Prussia mwaka 1945 mji ulikuwa sehemu ya jimbo la Saksonia-Anhalt.
Eisleben si mji tu wa kuzaliwa kwa Luther ni pia mahali alipohubiri mara ya mwisho wa kifo na kuaga dunia. Nyumba za kuzaliwa na kufa kwake ni mahali pa makumbusho zilizopokelewa katika orodha yaurithi wa dunia yaUNESCO.
Makala hii kuhusu maeneo yaUjerumani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuEisleben kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.