Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Einsteini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Einsteini inang'aa kwa rangi ya buluu wakati wa giza kutokana na unururifu wake

Einsteini (Einsteinium) nielementi ya kikemia yenyenamba atomia 99. Hiyo inamaanisha kuwakiini cha atomu yake huwa naprotoni 99 naelektroni 99. Nielementi sintetiki, maana haitokei kiasili, bali inategenezwa katikamaabara. Sababu niunururifu wake pamoja nanusumaisha yasiku 40 hadi 471 pekee.Isotopi zake zote ni nururifu, hazidumu.

Katikajedwali la elementi Einsteini huhesabiwa kati yaaktinidi ambako ina nafasi ya saba.Isotopi ya kudumu zaidi ya Einsteini ina protoni 99 naneutroni 153. Kuna isotopi 19 tofauti (zote nururifu).

Einsteini iligunduliwa mara ya kwanza mnamo1952 naAlbert Ghiorso natimu yake yawanasayansi waliochungulia takataka iliyobaki baada yamlipuko wabomu ya hidrojeni yakwanta, ikatambuliwa kama elementi katikaChuo Kikuu cha Kalifornia,Berkeley.

Jina lilichaguliwa kwakumbukumbu yamwanafizilia mashuhuriAlbert Einstein.

Hakuna matumizi ya kweli yanayojulikana nje yautafiti wa kisayansi.

Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuEinsteini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Einsteini&oldid=1106662"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp