Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Waraka kwa Waebrania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaEb)
Agano Jipya

Barua kwa Waebrania ni kati yavitabu 27 vyaAgano Jipya katikaBiblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vyaBiblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wahistoria ya wokovu ili kukielewa kadiri yamaendeleo yaufunuo waMungu kwabinadamu.

Mazingira

[hariri |hariri chanzo]

Miaka ya 60B.K.Mkristo mwenyeasili yaKiyahudi naelimu yaKiyunani, aliwaandikiaWakristo wa Kiyahudi wenzake sibarua hasa, balihotuba kamili iliyoambatanishwa na kipande cha barua.

Hali iliyosababishauandishi ni baadhi yao kuvutiwa tena nadini yao asili naibada zakehekaluni:kishawishi kilikuwa kikubwa hasa kwa sababuKanisa lilikuwa bado mwanzoni, bilamahali maalumu pa kusali wala ibada zafahari.

Mwandishi aliwaonya kuwa wakimuasiYesu hawamrudiiMungu aliye hai, aliyejifunua hasa katikaMwanae, baliwanamsulubisha tena kwa makusudi mazima na kustahili tumoto wa milele.

Mwandishi

[hariri |hariri chanzo]

Ingawa Waraka huu umehusianishwa na zile zaMtume Paulo, toka zamani ilijulikana kuwa mwandishi wake si yeye, ila mtu aliyeshirikiana naye. Kati ya wanaotajwa zaidi kunaBarnaba naApolo.

Mada

[hariri |hariri chanzo]
Kuhani Mkuu wa Agano la Kale alivyochorwa mwaka1821.

Sehemu kubwa yamaandishi hayo inalinganishaYesu Kristo naukuhani wake katikahekalu lambinguni upande mmoja, na ukuhani waAgano la Kale hukoYerusalemu upande mwingine.

Hivyo mwandishi alielekezasafari ya kiroho katikaimani inayofanana na ile yawatakatifu wa Agano la Kale.

Kwa kuwa lengo halikuwa la kinadharia, bali kuhimizauaminifu, kila baada ya kuchambuaukweli fulani aliongezamawaidha ya kufaa.

Ubora wa kitabu hiki

[hariri |hariri chanzo]

Ubora wake ni kulinganisha mambo ya kale na utimilifu wake katikaAgano Jipya, pia kuthibitisha ukuu waKristo kama kuhani wamilele (Eb 1:1-2:4; 4:11-5:10; 7:1-8:13; 10:19-11:40; 13:22-25). Hiyo inaendana naufasaha walugha.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  • Attridge, Harold W.Hebrews. Philadelphia, PA: Fortress Press, 1989.
  • Bruce, Frederick F.The Epistle to the Hebrews. New International Commentary on the New Testament. Grand Rapids: Eerdmans, 1964. Rev Ed 1990.
  • Guthrie, DonaldThe Letter to the Hebrews. Grand Rapids, MI: Wm. B. Eerdmans Publishing Co., 1983
  • Hagen, Kenneth.Hebrews Commenting from Erasmus to Beze. Tübingen: J.C.B. Mohr (Paul Siebeck), 1981.
  • Heen, Erik M. andKrey, Philip D.W., eds.Ancient Christian Commentary on Scripture: Hebrews. Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 2005.
  • Hughes, P.E.A Commentary on the Epistle to the Hebrews. Grand Rapids, MI: William B. Eerdmans Publishing Company, 1977.
  • Hurst, L. D.The Epistle to the Hebrews: Its Background of Thought. Cambridge:Cambridge University Press, 1989.
  • Koester, Craig R. "Hebrews". Anchor Bible 36. New York: Doubleday, 2001.
  • Lane, William L.Hebrews 1–8.Word Biblical Commentary Vol. 47A. Dallas, TX: Word Books, 1991.
  • Lane, William L.Hebrews 9–13.Word Biblical Commentary Vol. 47B. Dallas, TX: Word Books, 1991.
  • O'Brien, Peter T.The Letter to the Hebrews.Pillar New Testament Commentary. Grand Rapids: Eerdmans / Nottingham: Apollos, 2010.
  • Paul EllingworthReading through Hebrews 1–7, Listening especially for the theme of Jesus as high priest.Epworth Review 12.1 (Jan. 1985): 80–88.
  • Paul Ellingworth,The Epistle to the Hebrews. New International Greek Testament Commentary, Eerdmans, 1993

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]

Tafsiri ya Kiswahili

[hariri |hariri chanzo]
  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

Ufafanuzi

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuWaraka kwa Waebrania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Waraka_kwa_Waebrania&oldid=1322823"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp