Dunia ni mojawapo yasayari nane zinazozungukaJua letu katikaanga-nje. Kati ya sayari zaMfumo wa Jua, Dunia yetu ni sayari ya tatu kutoka kwa Jua.
Masafa baina yake na Jua nikilomitamilioni 150 aukizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka Jua, na masaa 23.9345 kuuzungukamhimili wake naupana wake ni kilomita 12,756.
Ni mahali pekee katikaulimwengu panapojulikana kunauhai ulioaminiwa kuanza miaka bilioni 3.5 iliyopita[3].
Uhai unapatikana kwaspishi milioni 10-14 zaviumbe hai pamoja nawanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7.2[4].
Umbo la Dunia
Umbo la Dunia linafanana natufe aumpira unaozunguka kwenye mhimili wake. "Mhimili wa Dunia" nimstari kati yancha zake.
Lakini si tufe kamili. Inauvimbe kidogo kwenye sehemu yaikweta; ilhaliumbali kati ya ncha mbili nikilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaanikipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha. Tofauti hii inasababishwa namzunguko wa Dunia.Kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali Duniani palipo karibu zaidi na anga-nje siMlima Everest kwenyeHimalaya balimlima Chimborazo nchiniEkuador.[5]
Kwenye uso wake Dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili. Nusu moja ina eneo kubwa lamabara yaaninchi kavu ambayo niasilimia 47 ya sehemu hii. Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji yabahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maeneo yake.
Kwa jumla Dunia ni sayari pekee katikaMfumo wa Jua yenyemaji katika hali yakiowevu usoni mwake.Bahari kuu ya Dunia inashika asilimia 96.5 ya maji yote yaliyopo Duniani. Maji ya bahari huwa na asilimia 3.5chumvi ndani yake.
Kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa Dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 zaAsia,Afrika,Amerika Kaskazini,Amerika Kusini,Antarktika,Ulaya naAustralia. (Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikiwa kamarasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama bara naGreenland kamakisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima).
Dunia jinsi inavyozunguka kwenye mstari wa mhimili wake
Maeneo ya bahari kuu ya Dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 zaPasifiki,Atlantiki naBahari ya Hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenyeMfereji wa Mariana katika Pasifiki (mita 11,034 chini ya UB). Kwawastani bahari huwa nakina cha mita 3,800.
Nusutufe ya Dunia yenye maji mengiMatabaka yaliyopo katika muundo wa Dunia.
Tumeona Dunia ina umbo la mviringo au tufe. Tufe hilo si kipande kimoja kikubwa chamwamba thabiti. Dunia ina muundo ndani yake. Muundo huo unafanana kiasi nakitunguu, yaani Dunia yetu imefanyika kwa matabaka mbalimbali yanayofuatana kutoka nje kwenda ndani. Kila moja lina tabia yake.
Kimsingiwataalamu hutofautisha matabaka matatu ambayo ni:
Ganda la Dunia ni sehemu imara na uhai wote tunaouJua unapatikana juu yake. Katikati hali ya koti na ya kiini ni ya joto kubwa sana namaada yake hupatikana katika hali yagiligili (si imara, kuyeyushwa). Kila ukiingia ndani Dunia inazidi kuwa yamoto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikianyuzi 5000-6000 °C.
Vipimo vimeonyesha ya kwamba matabaka mawili ya koti na kiini huwa tena na mgawanyiko ndani yake, hivyo matabaka yafuatayo yanaweza kutofautishwa.
Tabaka
Kuanzia kilomita
Ganda la nje
0 - 40
Koti la juu
40 - 400
Koti la kati
400 - 900
Koti la chini
650 - 2900
Kiini cha nje
2900 - 5100
Kiini cha ndani
5100-6371
Sehemu ya juu ya koti inafanana kikemia na ganda na sehemu hizo mbili zinaitwatabakamwamba. Tabakamwamba inaunene wa kilomita 50 - 100.
Tabakamwamba imekatika katika vipande vinavyoitwamabamba la ganDunia. Vipande hivi vinaelea juu ya giligili ya koti la ndani. Ndiyo sababubara lolote si lamilele; kilabamba huwa namwendo wake na ndiyo sababu katikahistoria ya Dunia mabara yameachana na kuungana mara kadhaa. Kwa mfano imepimwa ya kwamba sehemu kubwa yaAfrika ya Mashariki ina mwendo wa kuachana na bara la Afrika nadalili yake nibonde la ufa.
Tabia hiyo inasababishwa na mwendo wa mikondo ya chuma cha moto kilichoyeyuka katika kiini cha nje cha Dunia. Mistari ya nguvu ya sumaku inatoka nje kwenye ncha ya kusini na kurudi ndani ya Dunia kwenye ncha ya kaskazini. Tabia hiyo ni msingi wa kazi yadira ambamo sindano ya dira huvutwa daima na ncha sumaku ya Dunia na kuelekea kaskazini muda wote.
Ugasumaku wa Dunia nikinga muhimu kwa uhai wote Duniani. Dunia inapigwa muda wote namnururisho kutoka Jua kwa njia ya "upepo wa Jua". Mnururisho huo ninuru pamoja miale ya hatari. Ugasumaku unakengeusha sehemu kubwa ya mnururisho hatari hadi unapita kando ya Dunia na kutofika kwenye uso wa Dunia.
Dunia kama mahali pa uhai
Dunia yetu ni sayari pekee inayojulikana mpaka sasa ambapo binadamu na viumbe vingine vinaweza kuishi. Wanasayansi bado wanafanya ufafiti kuJua kama kuna kuna viumbe hai kwenye sayari nyingine.
Hapa kuna sababu mbili zinazofanya viumbehai kuishi Dunianiː
Dunia yetu ina umbali na Jua unaofaa kwa maisha kwa sababu sayari zilizoko karibu zaidi na Jua (k.m.Zuhura) zina joto kubwa mno na sayari zilizoko mbali zaidi kamaMrihi ni baridi mno.
Dunia yetu inaangahewa yenye asilimia 78 yanaitrojini, asilimia 21 yaoksijini na asilimia 1 ya aina nyinginezo zahewa, na kwa sababu hii uhai na maisha yanamakinika katika ardhi, kinyume na sayari nyinginezo.
Uso wa Dunia
Picha ya Dunia ikionyesha kutokea kwa mabara kutoka kugawanyika kwaPangea mpaka hivi leo.
Sehemu kubwa kabisa ya Dunia inafunikwa nabahari, kwani takriban asilimia 70 ya uso wake unafunikwa namaji ya bahari na kutokana na maji yote yaliyokuwepo ardhini, asilimia 97 ni maji ya bahari, na asilimia 3 nimaji matamu.Theluthi inayobaki ni nchi kavu kwenyemabara mbalimali na visiwa vingi.
Sura ya Dunia ni kilomita mraba 510,000,000, ikiwa nchi kavu imechukua eneo la kilomita mraba 149,430,000 na maji yamechukua eneo la kilomita mraba 360,570,000.
Hewa iliyoko juu ya ardhi vile vile ina matabaka mbalimbali, na kila tabaka lina kazi yake. Hewa kwa jumla ina masafa ya kiasi cha kilomita 560 aumaili 348 kuendea juu, na baada ya hapo unaingia kwenye anga-nje. Hewa hiyo ndiyo inayokinga viumbehai namadhara ya Jua na mnururisho wa angani ambao unaingia anga ya Dunia na kuteremka chini.
↑Schopf, JW, Kudryavtsev, AB, Czaja, AD, and Tripathi, AB. (2007).Evidence of Archean life: Stromatolites and microfossils. Precambrian Research 158:141–155.
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuDunia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.