Wataalamu kadhaa hujaribu kuona uhusiano kati ya mji wa "Ebalana" uliotajwa na katika maandiko yaPtolemeo mnamo 140 BK lakini hakuna uhakika kuhusu mahali pake.
Mji wa leo ulianzishwa kama kiji cha wavuvi kwa jina la „Áth Cliath“ na kando lake Wavikingi walijenga kijiji cha jirani cha „Dubh Linn“ ("matope mweusi"). Vijiji vikaungana na kuwa mji tangu 1172 kwa sababuWanormandi baada ya kuvamia Eire kutoka Uingereza walianzisha makao makuu yao hapa. Katika kipindi hadi karne ya 16 Dublin ilikuwa kitovu cha eneo lililokuwa chini ya wafalme wa Uingereza kisiwani na tangu 1541 mji mkuu wa Ufalme wa Eire uliotawaliwa na mfalme wa Uingereza.
Baada ya muungano wa Uingereza na Eire katikaUfalme wa Muungano Dublin ilikuwa makao ya gavana mwingereza.
Uhuru wa Eire ulianza1916 mjini Dublin kwenye uasi wa Pasaka. KwenyeVita ya Uhuru ya Eire nyumba nyingi ziliharibiwa.Tangu uhuru wa 1922 Dublin ikawa mji mkuu.
Baada ya kujiunga kwa Eire na Umoja wa Ulaya Dublin imeendelea kukua na kuwa jiji ya Kiulaya. 1998 Dublin ilisheherekea sikukuu ya kumaliza miaka 1000.