Dola la Roma Magharibi ni sehemu yaDola la Roma upande wa Magharibi iliyo na mji mkuu waRoma. Kuanzia mwaka wa285 Dola la Roma lilikuwa namakaisari wawili ili kurahisisha utawala wa en eneo lililokuwa kubwa mno.
Chini yaKonstantin Mkuu, mji waKonstantinopoli ulitangazwa mji mkuu wa pili. Baada ya kifo chaTheodosius Mkuu, utawala uligawanywa kati ya wana wake na kweli kulikuwa na madola mawili yenye miji mikuu miwili.
Katika magharibi wanajeshiWagermanik katika utumishi wa Waroma walipata uwezo zaidi hadi wakamua kushika madaraka wenyewe. Mtawala wa mwisho wa Roma Magharibi alikuwa KaisariRomulus Augustus aliyeondoshwa madarakani mwaka wa476. Mkuu wa jeshiOdoaker alimpindua Romulus akajitangaza kama mfalme wa magharibi hata akiendelea kuheshimu kipaumbele wa makaisari wa mashariki mjini Konstantinopoli.
Watawala Wagermanik wa Italia waliendelea kutawala katika jina la makaisari lakini hali halisi Dola la Roma Magharibi lilikuwa limekwisha.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuDola la Roma Magharibi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.