Dola Takatifu la Kiroma si sawa naDola la Roma la Kale.
Ramani ya Dola Takatifu la Kiroma yaonyesha mikoa yake.Maeneo ya Dola Takatifu la Kiroma pamoja na mipaka ya nchi za sasa.
Dola Takatifu la Kiroma (Kijerumani:Heiliges Römisches Reich,Kilatini:Sacrum Romanum Imperium) lilikuwa jina laUjerumani kati ya takriban mwaka1000 na1806. Lakini dola hilo, licha ya Ujerumani, lilikuwa pia na maeneo makubwa, yakiwa ni pamoja naAustria,Italia ya Kaskazini,Ubelgiji,Uholanzi naUcheki wa leo.
Mipaka yake yalibadilika mara kadhaa katikakarne nyingi za kuwako kwake.
Maeneo hayo yote yaliunganishwa chini yaKaisari aliyekuwa pia mfalme wa Wajerumani.
Maeneo hayo yalikuwa na kiwango kikubwa cha kujitegemea yakitawaliwa na makabaila wa ngazi mbalimbali na maaskofu waKanisa Katoliki au yakiwa miji huru.
Halikuwa dola la kisasa, kwa kuwavyombo vya dola vilikuwa vichache. Kaisari alitegemea hasa mali yake binafsi pamoja na haki ya kuthibitisha watu waliopokea vyeo mbalimbali.
Asili ya dola lilikuwa milki yaKarolo Mkuu aliyefaulu kuunganisha Ujerumani,Ufaransa na Italia chini yake. Mwaka800 alipokea cheo cha Kaisari wa Roma kutoka mikono yaPapa Leo III.
Hatua hii ilichukuliwa kama kuendelezwa kwa Dola la Roma la Kale katika magharibi ya Ulaya hata kama hali halisi ilikuwa kwamba milki ya Karolo ilikuwa milki yaWafranki naWagermanik wengine na taasisi zote zaRoma ya Kale zilikuwa zimeshakwisha kabisa katika magharibi ya Ulaya.
Lakini makaisari walijenga hoja la "translatio imperii" (kwa Kilatini: ukabidhi wa mamlaka) la kuwa mamlaka ya Kaisari yaliyokuwa na Waroma wa Kale na sasa yalikabidhiwa kwa Wajerumani.
Karolo aligawa urithi wake kati ya wanae na hii ilikuwa chanzo chaUfaransa upande wa magharibi na Ujerumani upande wa mashariki. Cheo cha Kaisari kiliendelea upande wa mashariki. Hivyo Ufaransa iliendelea kuwa ufalme wa nchi moja lakini upande wa mashariki Wajerumani waliunganishwa pamoja na watu jirani chini ya Kaisari aliyekuwa pia mkuu wa Italia ya Kaskazini,Bohemia (Ucheki) na sehemu mbalimbali ambazo leo hii ni ama Ufaransa au Ubelgiji na Uholanzi.
Mjerumani wa kwanza aliyepokea ukaisari kutoka kwaPapa waRoma alikuwaOtto I mwaka962.
Hadikarne ya 13 dola lilikuwa na nguvu. Baadaye maeneo ndani yake yalijiongezea kiwango cha kujitawala. Kila Kaisari alichaguliwa na kamati ya makabaila na watemi wakuu. Kabla ya uchaguzi Makaisari walipaswa kuahidi ya kwamba wataheshimu haki ya makabaila juu ya maeneo yao. Mwishoni maeneo yalikuwa kamanchi huru kabisa yaliyoendelea kujitawala, kuendeshavita dhidi ya majirani kufuatasiasa zao.
Mwishoni dola lilikuwa za zaidi ya maeneo 300 ya kujitegemea; mengine makubwa kama Austria naPrussia, mengine madogo mno yenye eneo lamji mmoja tu.
Lakini vita vya kuwasukuma Waturuki watoke katika maeneo ya Ulaya ya kusini-mashariki waliyowahi kuvamia viliendeshwa na Kaisari kama mkuu wa Austria bila ya msaada wa dola takatifu.
Dola lilifaulu kwa kiasi fulani kutunzaamani au angalau kuepuka vita kati ya maeneo yake. IsipokuwaVita ya Miaka 30 kati ya1618 na1648 ilionyesha uwezo mdogo wa dola na karibu theluthi moja ya wakazi wa Ujerumani walikufa.
Tangukarne ya 17 majirani kama Ufaransa naSweden walijiingiza zaidi na zaidi katika siasa ya Ujerumani na maeneo makubwa kama Prussia hayakujali tena maazimio ya Kaisari. Dola Takatifu likaendelea kudhoofika.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuDola Takatifu la Kiroma kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.