Delta hii inachukua kiasi chakilometa 249 zaufukwe wa bahari ya Mediterania na pia katika eneo hili hufanyika shughuli mbalimbali zakilimo. Kuanzia upande wa Kaskazini hadiKusini delta hii inakadiriwa kuwa naurefu wa kilometa 160. Delta hii inaanzia taratibu chini kuanzia katikamji waCairo.
Mto Nile na Delta
Wakati mingine delta hii, hugawanywa katika vijisehemu vya Mashariki na Mashariki. Huku mto Nile wenyewe ukigawa mikono mito miwili yaaniDamietta naRosetta. Ikiwa inatiririkia katika bahari ya Mediteranea pia huwa na majina hayohayo.
Zamani, delta hii ilikuwa na mikono mito mbalimbali, lakini mikono mito hii ilipotea kutokana na jitihada za kuzuiamafuriko, kwa kukinga na kubadilisha mwelekeo. Moja kati ya mikono mito iliyopotea ni ule waWadi Tumilat.
Mto Nile kutoka juu unaonekana kamapembetatu. Pande za delta hii zinaonekana kumong’onyoka na baadhi ya mikono mito inaonekana kupanuka wakati ikiwa inaingia katika bahari ya Mediterania. Kutokana na kujengwa kwabwawa laLambo la Aswan kumepunguza kuja kwarutuba katika maeneo ya delta na hivyo kusababishawakulima kutumiambolea nyingi ili kurejesha hali ya rutuba katika maeneo ya kufanyia shughuli za kilimo katika eneo la delta. Sehemu yaudongo wa juu katika eneo la delta ni karibu na hatua 70 kwenda chini.
Watu wamekuwa wakiishi katika eneo la delta ya mto Nile kwa miaka zaidi yaelfu kadhaa, na pia wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo cha hali ya juu. Mto Nile umekuwa ulifurika katika kipindi chamwaka angalau mara moja, lakini hali hii imekuwa ikipungua kutokana na kutengenezwa kwa bwawa la Aswan.Kumbukumbu za siku za kale zinaonesha kuwa, Delta imekuwa na milango mito kadhaa.
Kwa upande wa Mashariki hadi magharibi, milango mito ni kama, Tanitic, Mendesian, t Phatnitic au Phatmetic[1]), pia kuna milango mito ya Sebennytic, Bolbitine, na Canopic pia hujulikana kama Herakleotic. Kwa sasa kuna milango mito miwili tu, hii ni kutokana na jitihada za kuzuia mafuriko na kuporomoka kwa pande za milango mito, milango mito hiyo ni pamoja na: Damietta uliopo kwa upande wa Mashariki, na Mlango mto wa Rosetta[2]. Mlango mto huu wa Damietta upo upande wa Magharibi wa delta.
Rosetta Stone lilipatikana katika delta ya mto Nile mwaka1787, katikabandari ya Rosetta. Katika enzi zaFarao, Delta hii ilikuwa ikijulikana kamaMisri ya Chini na pia ilikuwa ikiitwa "Goshen". Pia kuna sehemu kadhaa za kihistoria katika eneo la delta.[3]
Katika kipindi cha mwisho wa mwaka eneo la mto Nile huwa lina mwonekano mwekundu na kuwa namaua yalotus flowers. Upande wa chini wa eneo la Nile, yaani upande wa Kaskazini, na upande wa juu yaani upande wa Kusini, kunamimea mbalimbali inayoota kwa wingi. Mimea inayoota kwa wingi katika eneo la Mto Nile kwa upande wa chini ni yale yanayoitwa Egyptian lotus, na kwa upande wa juu hujawa na mimea inayoitwaCyperus papyrus au (papyrus sedge), japokuwa mimea hii haioti kwa wingi wakati huu kama ulivyokuwa hapo awali.
Wanyama wengine wanaopatikana katika eneo la delta ya Nile ni pamoja navyura,hua,kobe nanguchiro, lakini pia kunamamba naviboko: wanyama hawa wawili walikuwa wameenea sana katika eneo la delta katika siku za nyuma lakini siku hizi hali haipo hivyo. Aina zasamaki wanaopatikana katika eneo la delta ni pamoja na samaki wa aina yaStriped mullet.
Delta ya mto Nile inatabia za Kimediterania, ambayo huwa na sifa yamvua kidogo, kiais chamililita 100 hadi 200 kwa wastani wa mwaka na hata hivyo mvua hizi hunyesha wakati wa miezi yabaridi. Eneo la delta huwa na kipindi chajoto katika miezi yaJulai naAgosti kiasi chanyuzijoto 30 °C hadi nyuzijoto 48 °C. Kipindi cha baridi huwa ba kiasi cha nyuzijoto 10° hadi 19 °C. Eneo la delta huwa na hali yaunyevunyevu katika kipindi cha miezi ya baridi. Eneo la Delta limekuwa likimong’onyoka kwa wastani wa kilometa 502 kwa mwaka{{Fact|date = Aprili 2008 na inatabiriwa kuwa eneo la delta litakuwa limeisha hadi kufikia mwaka2550.