Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Delta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Delta yaMto Nile inavyoonekana kutoka angani - picha yaNASA

Delta (kutokajina laherufi yaalfabeti ya Kigiriki) nimdomo wamto wenyeumbo la kufanana naherufi ya Kigiriki Δ (=delta) sawa napembetatu.

Kutokea kwa delta ya mto

[hariri |hariri chanzo]

Umbo hili hutokea kamamaji ya mto yanabebamatope,mchanga namashapo mengine hadi mdomo wakebaharini auziwani. Maji ya mto yakiingia baharini hupunguza mwendo wake nanguvu ya kubeba yaliyomo ndani yake. Mashapo yanashuka chini: kwanza sehemu zake nzitonzito kamachangarawe, halafu mchanga, halafuudongo. Mashapo hayo yanalalaganda baada ya ganda na kuimarika hadi kuonekana juu yauwiano wa maji. Sehemu hizo za mashapo yaliyoimarika zinakuwa kama kizuizi kinacholazimisha mto kugawa mwendo wake. Kwa njia hiimikono mbalimbali inatokea.Mimea inaanza kukua kwenye nchi mpya ikiwamizizi yao inashika na kuimarisha nchi hii.

Mto unaendelea kupeleka mishapo yake mdomoni na kujenga delta yake ndani ya bahari jinsi inavyoonekana kwenyemto Nile ambako delta imetoka nje yamstari wapwani.

Ikiwa bahari ina tofauti kubwa kati yamaji kujaa na kupwa mdomoni mwa mto tena bahari hainakina kubwa hutokea mlango wa mto wenye umbo la V (kama faneli) kwa sababu mwendo wa maji kujaa na kupwa unazuia kutelemka na kuimarika kwa mashapo.

Mito mikubwa yenye mdomo wa delta

[hariri |hariri chanzo]

Pamoja na mto Nile kuna mito mingi mikubwa yenye mdomo wa delta:

Delta ya barani

[hariri |hariri chanzo]
Korongo Domo-ngazi wawili kwenye mkono moja wa delta ya barani ya Okavango.

Wakati mwingine delta inatokeabarani pasipo bahari. Kuna hasa ainambili: ama mto unakwisha barani (hasa kama nijangwa) au mto unaendelea.

HukoMali kuna delta ya barani ya mto Niger; mto unajigawa kwa mikono mbalimbali katika eneo kubwa la maziwa na maeneo ya matopematope.

MtoOkavango unakwisha kwenye delta yake katika jangwa laKalahari (Botswana). Delta hii ni eneo lenye mimea nawanyama wengi katikati ya jangwa kubwa. Delta inavutawatalii wengi kilamwaka.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Delta&oldid=1045951"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp