Silva ana uwezo wa kucheza kwa upande wowote au kama namba 10 ya kiasili, na wakati mwingine kama mshambulizi msaidizi. Ni mchezaji mwenye mwili mdogo, na mara nyingi hulinganishwa na Aimar Pablo, alipochukua nafasi yake huko Valencia, akivalia nambari iliyohusishwa sana na Aimar; namba 21.
Silva alianza kucheza mpira wa kulipwa msimu wa 2004-05 katika Ngazi ya pili katika timu ya SD Eibar, akiwa amekopwa kutoka Valencia CF na alicheza mechi 35 katika daraja hilimna kufunga mabao matano. Msimu uliofuatia, alikopwa tena, lakini wakati huu alikopwa na timu ya Celta de Vigo, ambapo alicheza mechi 34, na kufunga mabao manne. Baada ya kucheza mechi mbili ambazo aliingia uwanjani katika dakika za mwisho za mechi hizo, ambapo mechi ya kwanza iliisha kwa Celta de Vigo kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Malaga CF tarehe 28 Agosti 2005. Silva akamaalizia msimu huo kama mshambulizi bora huku timu hii ya Kigalisia ikifuzu katika kombe la UEFA moja kwa moja kutoka daraja la pili.
Katika misimu miwili, alikosa kucheza mechi sita tu ilhali alifunga mabao 14 (bao la kwanza alilifunga tarehe 5 Novemba 2006 katika tasa ya 1-1 ugenini RCD Espanyol).
Baada ya kutocheza kwa muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la kisigino ambapo alifanyiwa upasuaji, Silva alirejea kikosini katikati mwa Desemba.[1]
Silva aliwakilishwa Uhispania akiwa na Cesc Fabregas mara ya kwanza mwaka wa 2003 katika michezo ya ubingwa duniani ya FIFA ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 huko Finland, ambapo alifunga mabao matatu. Mwaka wa 2006, alijiunga na timu ya Uhispania ya wachezaji wasiozidi umri wa 21 na alifunga mabao manne katika kombe la vijana duniani la FIFA mwaka 2005; hii ilimwezesha kunyakua nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji bora, pamoja na mshambulizi mwitaliano Graziano Pellè.
Silva alichezea mara ya kwanza timu kuu ya Uhispania tarehe 15 Novemba 2006 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Romania ambapo timu yake ilishindwa 1-0 nyumbani. Aliendelea kutajwa katika orodha ya timu ya Uhispania baada ya kuchangia vizuri katika mechi zake za kwanza. Tarehe 22 Agosti 2007, Silva aliifungia Uhispania mabao yake ya kwanza kikosini mwa Uhispania, na alifunga mara mbili katika mechi hiyo ambapo waliishinda Ugiriki 3-2 katika mechi ya kirafiki. Baadaye aliitwa ajiunge na kikosi cha wachezaji 23 ambao wangeiwakilisha nchi yao katika dimba la Euro 2008.
Katika nusu fainali Silva alifunga bao la tatu la Uhispania dhidi ya Urusi baada ya ushambulizi wa haraka ambayo Cesc Fabregas alimpigia krosi Silva, ambaye alitia mpira ndani ya lango la Igor Akinfeev kwa kutumia mguu wake wa kushoto.
Katika fainali, Silva alihusika katika tukio fulani na mjerumani Lukas Podolski. Baada ya kumvuta Podolski chini, Podolski alimwenedea Silva na kuzua ubishi mkali ambao haukuadhibiwa na mwamuzi. Muda mfupi baadaye, kocha wa timu ya Uhispania, Luis Aragonés, alimwondoa Silva na kuleta Santi Cazorla ili kuzuia wezekano la vita.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuDavid Silva kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.