Jengo la Bunge (Assemblée Nationale)Ramani ya mitaa ya Dakar
Dakar nimji mkuu waSenegal ikiwa na wakazi 2,352,000. Iko kwenye rasi la Verde ambalo ni pembe la magharibi yaAfrika. Bandari yake ina nafasi nzuri kwa biashara naUlaya naAmerika.
Mji ulianzishwa naWafaransa mwaka 1857 walipoondoka kisiwa chaGoree kuhamia bara. Ukapata bandari ya biashara na pia bandari ya kijeshi halafu ukawa mwanzo wa reli katika Senegal. Mwaka 1902 Dakar ilikuwa mji mkuu wa Afrika ya Magharibi ya Kifaransa badala yaSaint-Louis. Kati 1959 hadi 1960 ilikuwa mji mkuu waShirikisho la Mali, baadaye mji mkuu wa Senegal.
Kisiwa cha Goree ambacho sasa ni sehemu ya mji kilikuwa kati ya vituo muhimu vyabiashara ya watumwa. Boma la Fort D'EstreesGorée kisiwani humo lilikuwa gereza la watumwa kabla ya kupelekwa kwenye meli na leo ni makumbusho.