Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

DNA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa mfumo wa DNA.

DNA nikifupisho chaDeoxyriboNucleic Acid ambayo nijina laKiingereza lamolekuli kubwa ndani yaseli zaviumbehai wote. KwaKiswahili huitwaAsidi DeoksiriboNukleini (kifupi:ADN) auAsidi Kiinideoksiribo[1]; DNA hubebavinasaba (jeni) yaani sehemu ambazo zinaamua tabia za kiumbe husika kama vile mwonekano, jinsia, na yale yote kilichopokea kutokawazazi wake.

Wanyama,mimea,bakteria navirusi vilevile, wote wana DNA. Molekuli hii inabeba ndani yake habari zote zaurithi wa kiumbehai husika, yaani habari zatabia zote zinazopokewa kutoka kwa wazazi. Mwenye DNA zimojeni zinazotunza habari maalumu juu ya urithi wa kiumbe.

Molekuli ya DNA inaumbo kamangazi mbili za kupanda zilizounganishwa pamoja na kupindika kamasukurubu. Kila ngazi ninukleotidi ambayo ni muungo wasukari fulani pamoja namoja kati yabesi oganianne. Ufutano wa besi hizo unaamua namna ya kutengenezaprotini wakati wa kujenga seli mpya.

DNA ina uwezo wa kujinakili. Wakati wa kuzaa DNA inajipasua katikati ya pande mbili za "ngazi" yake. Hivyonusu "ngazi" ya upande wamzazi mmoja inaungana na nusu "ngazi" ya mzazi mwingine.

Tabia kamaukubwa,rangi yangozi aunywele ziko kila moja mahali pake; zikiunganishwa zababa namama,kemia inaamua ni upande gani wenyeathira zaidi na hivyo utajitokeza kwamtoto.

DNA inatokea hasa ndani yakromosomu kwenyekiini cha seli.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia iliyotolewa naTUKI inaandika "asidi kiinidioksiribo". Inapendekezwa kutumia -deoksi- badala ya -dioksi- kwa sababukiambishi de- inamaanisha "bila" (bila oksijeni) ilhali di- inamaanisha "mbili".

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuDNA kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=DNA&oldid=1257411"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp