Cirta, inajulikana pia kwa majina tofauti, zamani ilikuwa na makazi yaWaberber naWaroma wa kale ambao baadaye ulikuja kubadilishwajina na kuitwaConstantine, leo nchiniAlgeria.
Cirta ulikuwamji mkuu waufalme waKiberber waNumidia;mji wake muhimu uliopangiwa kimkakati kamabandari uliitwa Russicada. Ingawa Numidia ilikuwa na uhusiano muhimu najamhuri ya Roma kipindi chavita vya Karthago (264 -146KK), mji Cirta ulikuwamhanga wauvamizi kipindi chakarne ya 1 na2 kabla yaKristo. Hatimaye uliangukia chini yautawala wa Kirumi wakati wakaisariJulius. Cirta ulitawaliwa naWarumi katika kipindi cha Kaisari na chaAugustus na ulizungukwa na maeneo ya "shirikisho la miji huru ya Roma" kamaChullu,Rusicade, naMilevum, uliongozwa mwanzoni na Publius Sittius.
Mji uliharibiwa mwanzoni mwakarne ya 4 ukajengwa upya na kaisari waRomaKonstantino Mkuu, ambaye aliupa mji huo jina jipya la Constantine.Wavandali waliuharibu mji wa Cirta, lakini kaisariJustinian I akaunyakua na kuurekebisha mji huo wa Waroma.
Uliipungua umuhimu wake baada ya uvamizi waWaislamu, lakini jamii ndogo iliendelea kwa muda wakarne kadhaa.Magofu yake yamefanywa kamamakumbusho yakihistoria.
![]() | Makala hii kuhusu maeneo yaAlgeria bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuCirta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |