Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Chuo Kikuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chuo Kikuu cha Bologna (Italia) kilikuwa chuo kikuu cha kwanza chaUlaya.
Nyumba ya Hekima mjiniBaghdad (Iraki) ilikuwa kati ya watangulizi wa vyuo vikuu katika dunia yaKiislamu tangu mwaka800BK.

Chuo Kikuu nitaasisi yaelimu ya ngazi ya juu ambako wanafunzi wanafundishwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao hufundisha pamoja na kuendeshauchunguzi wa elimu mpya.

Wanafunzi husoma kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kupata elimu hadi kupita mitihani yashahada au digrii kama vile yabachelor (ya kwanza), ya uzamili (master) (ya pili) na yauzamivu, PhD (ya tatu).

Sifa

[hariri |hariri chanzo]

Siku hizi chuo kikuu kinatakiwa kuwa na sifa kadhaa za kukitofautisha na vyuo au taasisi nyingine kama vile:

  • kuunganisha fani mbalimbali kwa kukitofautisha na vyuo vinavyofundisha fani moja tu; kwa mfano chuo chaualimu, chuo chateolojia, chuo chauganga. Hata hivyo kuna vyuo vikuu vinavyokazia na kufundisha hasa upande mmoja wa elimu
  • kuunganisha kazi ya kufundisha na kazi ya uchunguzi kwa kukitofautisha na taasisi za uchunguzi zisizolenga mafundisho ya wanafunzi wa kawaida isipokuwa kuna nafasi ya kupata udokta
  • kutoa mafundisho ya ngazi ya juu inayokubaliwa kimataifa
  • kwa kawaida chuo kikuu kinatakiwa na kiwango kikubwa cha kujitawala nauhuru wa taaluma. Hali halisi hii inategemeamazingira: kuna tofauti kubwa kati nchi na nchi. Kufaulu katika maendeleo ya uchunguzi kunahitaji uhuru wa kuangalia, kuelewa na kujadili mawazo nafikra kutoka pande zote zadunia hata kama mawazo kadhaa hayakubaliwi katika mfumo wa kisiasa au kijamii ya nchi yenyewe.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Jamii katika tamaduni mbalimbali zilianzisha taasisi maalumu kwa elimu ya ngazi ya juu. Kati ya vyuo vya kwanza vinayofanana kiasi na chuo kikuu cha kisasa kuna hasa taasisi katikaUhindi,Ugiriki ya Kale,Uajemi,Ulaya na nchi za Kiislamu.

Mfumo wa kufundisha na kuratibu elimu ulio msingi wa vyuo vikuu vya kisasa ulianza hasa katika Ulaya yakarne za kati.

Vyuo hivi vya Ulaya viliendelea kuwa mahali pamaendeleo na kukuzasayansi ya kisasa. Kutoka hapa mfumo wa chuo kikuu pamoja na utaratibu wa ngazi zake za elimu ulisambaa kote duniani.

Madrasa ya Sankore mjiniTimbuktu.

Vyuo vikuu vya Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Kitovu cha kwanza cha elimu ya hali ya juu baraniAfrika kilikuwamaktaba ya Aleksandria nchiniMisri lakini ilikuwa taasisi ya kukusanya vitabu na mahali pa uchunguzi, si mafundisho.

Kihistoria vyuo vya kwanza vilivyotoa mafundisho kwenye hali ya juu ya kimataifa ya wakati wake vilikuwa chuo chaAl-Karaouine mjiniFes,Moroko tangu mwaka859 BK naAl Azhar mjiniKairo,Misri tangu mwaka975.

Upande wa kusini kwa Sahara niMadrasa ya Sankore mjiniTimbuktu (Mali) iliyotoa mafundisho ya hali ya juu kuanzia takriban mwaka1400.

Vyuo vikuu vya kisasa vilianzishwa nawamisionari katikakarne ya 19 nchiniSierra Leone naAfrika Kusini; vilianzishwa kama vyuo vya ualimu na kuendelea kuwa vyuo vikuu kamili.

Chuo Kikuu cha kwanza katikaAfrika ya Mashariki kilikuwaChuo Kikuu cha Makerere ambacho ni chuo mama cha vyuo vyaNairobi naDar es Salaam.

Vyuo vikuu bora barani Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Siku hizi ni hasa vyuo vikuu vya Afrika Kusini vinavyothaminiwa kuwa bora katika bara la Afrika.

Orodha ya utathmini wa vyuo vikuu bora barani Afrika kwa mwaka2013 ilikuwa kama ifuatayo:

  1. University of Cape Town,Afrika Kusini
  2. University of Pretoria,Afrika Kusini
  3. Universiteit Stellenbosch,Afrika Kusini
  4. University of the Witwatersran d,Afrika Kusini
  5. University of Johannesburg,Afrika Kusini
  6. University of KwaZulu-Natal,Afrika Kusini
  7. Rhodes University,Afrika Kusini
  8. The American University in Cairo,Misri
  9. North-West University,Afrika Kusini
  10. University of ,Ghana
  11. University of Nairobi,Kenya
  12. Mansoura University,Misri
  13. Cairo University,Misri
  14. University of the Western Cape,Afrika Kusini
  15. Tshwane University of Technology,Afrika Kusini

Kufikia mwaka 2016, vyuo vikuu kumi bora ni vyote vya Afrika Kusini.[1]

Majereo

[hariri |hariri chanzo]
  1. University Web Rankings - Africa
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Chuo_Kikuu&oldid=1430617"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp