Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Chuma cha pua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Daraja la reli nchini Argentina ilitengenezwa kwa kutumia feleji.
Mnara wa Eiffel mwenye kimo cha mita 300 ilikuwa jengo kubwa la dunia; imetengenzewa kwa chumapua tu.
Chumapua moto katika hali ya kiowevu yamwagwa kutoka jiko lake.

Chuma cha pua (pia:chumapua,feleji) nialoi wachuma pamoja na gredi mbalimbali zakaboni ambayo imekuwauti wa mgongo wamapinduzi ya viwandani. Hadi leo nimsingi wamashine navifaa vingi, piasilaha zinazounda uwezo wa kijeshi wamataifa. Piaujenzi wa kisasa hauwezekani bila chuma cha pua.

Chuma cha pua ni ngumu kushindachuma tupu isiyo nakaboni. Siku hizi kuna pia aloi za chumapua ambamodutu tofauti na kaboni hutumiwa.

Historia ya chumapua

[hariri |hariri chanzo]

Kutengenezwa kwa chumapua kulikuwasanaa ya pekee kwakarne nyingi. Silaha kamapanga za chumapua zilikuwa bora kushinda panga za chuma cha kawaida. Vilevile vifaa kamavisu hatamajembe vilidumu kama vilitengenezwa kwa chumapua.Wahunzi walipeana mbinu za kutengeneza chumapua kamasiri, kwa mfano kati ya wahunzi wajadi waWahaya wa maeneo karibu naZiwa Viktoria[1].

Tangumwaka1610viwanda katikaUingereza vilianza kutengeneza chumapua kwa vingi ikaboreshwa katika miaka 100 iliyofuata. Mbinu hiyo ilikuwa msingi wamaendeleo ya Uingereza juu ya mataifa mengine mengi katika mapinduzi wa viwandani. Mashine zote zilitengenezwa kwa chumapua.

Mnara wa Eiffel ulikuwajengo kubwa la kwanza lililoundwa kwa chumapua pekee.Meli za chumapua zilichukua nafasi yajahazi za awali zaubao.

Tabia za chumapua

[hariri |hariri chanzo]

Tabia za chumapua hutegemea na kiasi cha kaboni ndani yake. Kiasi kikubwa cha kaboni husabibisha aloi kuwa ngumu zaidi lakini inavunjika kwa urahisi pia. Kiasi kidogo cha kaboni husababisha chumapua kuwa laini zaidi lakini inanapukia zaidi.

Chumapua cha kawaida huhitaji kinga dhidi yakutu kama vilerangi au kupakwa kwazinki.

Nyongeza za kromi zababisha chumapua kutoshika kutu. Hivyo vyombo vyachakula kama vile nyuma, visu auvijiko hutengenezwa na aloi hiyo, pia vifaa vyamadaktari kama vile visu vyaupasuaji.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Peter Schmidt and Donald H. Avery: Complex Iron Smelting and Prehistoric Culture in Tanzania, Science Journal, New Series, Vol. 201, No. 4361 (Sep. 22, 1978), pp. 1085-1089online hapa

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuChuma cha pua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Chuma_cha_pua&oldid=1096391"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp