Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kodata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaChordate)
Kodata (Chordata)
Ugwe wa neva wa samaki huyu (Pristella tetra) uonekana kupitia ngozi
Ugwe wa neva wasamaki huyu (Pristella tetra) uonekana kupitia ngozi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Nusuhimaya:Eumetazoa
Faila ya juu:Deuterostoma (Wanyama ambaoblastospori yao inakuwamkungu)
Faila:Chordata
Kladi:Bilateria (Wanyama wenyeuenzipacha)
Ngazi za chini

Nusufaila:':

Muundo wa kodata (samaki sahili): 1 = uvimbe wa ugwe wa neva ("ubongo"), 2 =notokodi, 3 = ugwe wa neva, 4 =mkia nyuma ya mkungu, 5 =mkungu, 6 = njia ya chakula, 7 = mfumo wa mzunguko, 8 =atriopori, 9 = uwanda kuzunguka koromeo, 10 = ufa watamvua, 11 =koromeo, 12 = uwanda wa mdomo, 13 = minyiri, 14 =mdomo, 15 =gonadi (ovari/kende), 16 =jicho sahili, 17 =neva, 18 = mkunjo watumbo, 19 =ini sahili

Kodata (kutokalugha ya kisayansi:Chordata) ni kundi kubwa lawanyama wenyeugwe wa nevamgongoni.

Ugwe unaunganishaneva ambazo ni muhimu kwamwili kwa jumla na neva za kila sehemu au kiungo zinatoka hapa. Ugwe wa neva unaenda sambamba namhimili waseli ambazo ni imara zaidi amagegedu aumfupa.

Mhimili huu ni chanzo chauti wa mgongo kwa wanyama wengi wa kundi hili nakiunzi cha mifupa cha ndani ya mwili.

Kodata waliendelea kutoka kwa wanyama wengine kamaArthropoda wenyekiunzi cha nje.

Katikauainishaji wa kisayansi Kodata nifaila ya wanyama (Animalia).Nusufaila yenyespishi nyingi niVertebrata. Hapa mhimili wa kati unaendelea kuwa uti wa mgongo.

Samaki,amfibia,reptilia namamalia nioda ndani ya vertebrata.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Branchiostoma lanceolatum (Cephalochordata)
    Branchiostoma lanceolatum (Cephalochordata)
  • Rhopalaea sp. (Tunicata)
    Rhopalaea sp. (Tunicata)
  • Mikunga-ute (Hyperotreti)
    Mikunga-ute (Hyperotreti)
  • Salamanda mabaka-njano (Vertebrata)
    Salamanda mabaka-njano (Vertebrata)
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuKodata kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kodata&oldid=1244936"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp