Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Ujerumani (kwaKijer. Sozialdemokratische Partei Deutschlands auSPD,Kiing.Social Democratic Party of Germany) nichama cha siasa nchiniUjerumani kilichoundwa mnamo23 Mei1863. SPD ni kimoja kati ya vyama vya kisiasa muhimu zaidi katika Ujerumani ya sasa, pamoja naChama cha Kidemokrasia cha Kikristo (CDU).
SPD ilianzishwa kama "Shirika la Wafanyakazi wa Kijerumani" (Allgemeiner Deutscher Arbeiterverein, ADAV) mnamo 23 Mei 1863 hukoLeipzig.Mwanzilishi alikuwa Ferdinand Lassalle. Mnamo1875 ADAV ilijiunga na Chama cha Wafanyakazi wa Kidemokrasia ya Jamii (Sozialdemokratische Arbeiterpartei ) (SDAP), ambayo ilianzishwa mnamo1869 huko Eisenach na August Bebel na Wilhelm Liebknecht.
Jina jipya lilikuwa Chama cha Wafanyakazi cha Kijamaa cha Ujerumani (Sozialistische Arbeiterpartei Deutschlands, SAP).
Tangu mwaka1890 kilichukua jina lake la sasa.
Katika miaka kuanzia 1875 hadi 1890 kilipigwa marufuku naOtto von Bismarck.
Baada ya kuruhusiwa tena SPD ilikuwa mara kwa mara chama kikubwa zaidibungeni lakini haikushirikishwa katikaserikali yoyote. Wabunge wake, hasa Karl Liebknecht, walipingasiasa yaukoloni ya Ujerumani.
Baada ya kuanzishwa kwaVita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka1914, SPD iliona farakano. Wabunge walio wengi walikubali makisio ya pekee kwa ajili yajeshi wakiamini Ujerumani ilishmabuliwa, ilhalikundi dogo zaidi lilikataa makisio wakipinga kushirikivita vyovyote. Kundi hilo lilianzisha chama cha USPD ("SPD ya kujitegemea") kilichopinga vita.
Mwisho wa vita mnamo mwaka1918,mapinduzi yaliondoa utawala wa kifalme na SPD ikaongoza serikali kadhaa.
Wakati wamdororo mkuu wa uchumi baada ya mwaka1929, vyama adui wademokrasia vilipata nguvu katika Ujerumani. Mwaka1933 SPD kilikuwa chama pekee katika bunge kilichokataa kukubali "sheria ya mamlaka" (Ermächtigungsgesetz) iliyokuwamsingi wa kisheria kwaudikteta waAdolf Hitler.
Baadaye Hitler alipiga tena SPF marufuku na kuwakamata wanachama wengi, wengine walikimbia nje ya nchi.
Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia, SPD ilirudi. KatikaUjerumani ya Mashariki watawalaWasovyeti walilazimisha maungano ya SPD nachama cha Kikomunisti na kukamata wanachama waliopinga.
KatikaMagharibi mwa Ujerumani SPD iliendelea kama chama kikubwa zaidi ya mrengo wa kushoto.
SPD iliongoza serikali kadhaa zamajimbo huko Ujerumani Magharibi, lakini kila wakati ilikuwa chama kikuu cha upinzani katika bunge lashirikisho.
Iliingia katika serikali mara ya kwanza mnamo1966 chini yachanselaKurt Georg Kiesinger wa chama chaCDU.
Mnamo1969mwenyekiti wa SPDWilly Brandt aliweza kuunda serikali pamoja na chama kidogo cha kiliberali FDP. Chini yauongozi wake, Ujerumani ya Magharibi iliweza kujengaupatanisho naPolandi na kutambua mipaka mipya iliyowahi kutokea baada ya Vita Kuu ya Pili ambako Ujerumani ilipungukiwa maeneo makubwa. Brandt alifuatwa1974 na mwana SPD mwingine,Helmut Schmidt katika uongozi wa serikali.
Miaka1982 hadi1998 SPD iliondoka katika serikali ikawa tena chama cha upinzani.
Kati ya 1998 na2005 SPD iliweza kurudi katika uongozi wa serikali chini ya chanselaGerhard Schröder aliyeshiriki na chama cha kiekolojia cha Green Party.
Tangu Novemba 2005 hadi mwaka2021 SPD ikawa mshirika mdogo katika ushirikiano na CDU chini ya chanselaAngela Merkel .
Katika miaka hiikura za SPD katika chaguzi kwenye shirikisho na majimbo ziliendelea kupungua. Lakini katikauchaguzi mkuu wa mwaka 2021 SPD ilikuwa tena chama kikubwa kwa kupata kura zaidi kidogo kuliko CDU.
Kihistoria SPD ilikuwa chama chawafanyakazi nchini Ujerumani kilichofuata shabaha yaujamaa ambapoviwanda vikubwa vitawekwamikononi mwa serikali. Mnamo 1959 SPD iliachana rasmi naitikadi yaUmaksi ikakubaliuchumi wa soko (ambapo watu nakampuni zinaweza kutawalamali ya kila aina na kulengafaida yake kwenyesoko la uchumi) ikidai kwamba nguvu yauchumi wa binafsi inatakiwa kujenga manufaa yajamii yote. Hivyo ni kazi yadola kuwasaidia wanyonge kwa misaada ikiwa hawana kazi, niwagonjwa auwazee). Kampuni zinaweza kupataruzuku ili kuzisaidia ziendelee katika hali ngumu ili wafanyakazi wasikoseajira namishahara.
- Carl E. Schorske,German Social Democracy, 1905-1917: The Development of the Great Schism (Harvard University Press, 1955).
- Vernon L. Lidtke,The Outlawed Party: Social Democracy in Germany, 1878-1890 (Princeton University Press, 1966).
- Abraham J. Berlau,The German Social Democratic Party, 1914-1921 (Columbia University Press, 1949).
- Erich MatthiasThe Downfall of the Old Social Democratic Party in 1933 pages 51–105 fromRepublic to Reich The Making of the Nazi Revolution Ten Essays edited by Hajo Holborn, (New York: Pantheon Books, 1972).