Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Castor na Pollux

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jozi ya sanamu za Kirumi (karne ya 3 BK) zinazoonyesha Dioscuri kama wapanda farasi.

Castor na Pollux walikuwa mapacha katikaMitholojia ya Kigiriki namitholojia ya Kiroma. Pamoja wanaitwaDioscuri . Walikuwa wana wa malkia Leda wa Sparta. Dada zao walikuwa mabinti mapachaHelena wa Troia naKlitemnestra . Castor na Pollux walibadilishwa kuwakundinyota linalojulikana kwa jinaMapacha (ing. Gemini).

Ingawa walikuwa mapacha walizaliwa na mababa wawili tofauti: Baba wa Castor alikuwa binadamu Tindareus, mfalme wa Sparta na hivyo Castor alikuwa binadamu pia akijulikana atakufa, wakati baba wa Pollux alikuwa munguZeus kwa hiyo alikuwa na tabia ya kimungu asiyeweza kufa. Katika masimulizi ya Wagiriki mama Leda alilala na mumewe na siku ileile alitongozwa na Zeus kuzini naye ilhali Zeus alifika kwa umbo labatamaji.

Moja ya hadithi maarufu zaidi kuhusu Castor na Pollux ni jinsi walivyopelekwa angani kuwa kundinyota. Wakati wa vita fulani Castor mwenye tabia ya kibinadamu aliuawa. Pollux alihuzunika kupita kiasi akamwomba Zeus amfanye Castor asife ambayo ilimaanisha Pollux atalazimika kukupungukiwa tabia yake ya kimungu. Hatimaye, Zeus alikubali ombi hilo, kwa kuwapeleka wote wawili angani kama nyota. Walipangwa kukaa nusu mwaka kenyemlima Olimpos pamoja na miungu wengine lakini nusu mwaka wangekaa katika himaya ya mauti.


Kujisomea

[hariri |hariri chanzo]
  • "The Divine Twins in early Greek poetry". Robbins, Emmet.Thalia Delighting in Song: Essays on Ancient Greek Poetry. University of Toronto Press. 2013. pp. 238-253.ISBN 978-1-4426-1343-0
  • Lippolis, Enzo. "RITUALI DI GUERRA: I DIOSCURI A SPARTA E A TARANTO." Archeologia Classica 60 (2009): 117-59. www.jstor.org/stable/44367982.
  • De Grummond, Nancy Thomson. "Etruscan Twins and Mirror Images: The Dioskouroi at the Door." Yale University Art Gallery Bulletin, 1991, 10-31. www.jstor.org/stable/40514336.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Search WikisourceWikisource has the text of the1911 Encyclopædia Britannica articleCastor and Pollux.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Castor_na_Pollux&oldid=1196423"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp