Caracas(tamka: karakas) nimji mkuu waVenezuela. Mji uko katika kaskazini ya nchi karibu nabahari ya Karibi katika kimo cha 920m juu yaUB. Idadi ya wakazi ni kati ya milioni 3 au 4.
Mji uliundwa na MhispaniaDiego de Losada tar.25 Julai1567 kwenye mahali pa kijiji cha Kiindio cha Catuchacao kwa jina la Santiago de León de Carácas.
Mji ulikua tangu1750 kutokana na kilimo na biashara ya kakao.
Baada ya uhuru wa Venezuela mwaka 1831 ilikuwa mji mkuu wa jamhuri mpya.
Idadi ya wakazi ilikua polepole katika karne ya 19 hadi kufikia takriban 90,000 mnamo1900.
Baada ya kupatikana kwa mafuta ya petroli nchini uchumi ulipanuka na kuvuta wakazi wengi wapya.
Mitaa ya vibanda inapatikana kwenye mitelemko wa milima
Makala hii kuhusu maeneo yaAmerika Kusini bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuCaracas kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.