Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ngamia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaCamelus)
Ngamia
Ngamia nundu-moja (Camelus dromedarius)
Ngamia nundu-moja
(Camelus dromedarius)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia(Wanyama)
Faila:Chordata(Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli:Mamalia(Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda:Artiodactyla(Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda:Tylopoda(Wanyama wenye miguu inayovimba)
Familia:Camelidae(Wanyama walio na mnasaba nangamia)
J. E. Gray, 1821
Jenasi:Camelus(Ngamia)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 2:

C. bactrianusLinnaeus, 1758
C. dromedariusLinnaeus, 1758

Ngamia niwanyama wakubwa wajenasiCamelus katikafamiliaCamelidae inayowajumlisha pamoja nalama navikunya waAmerika Kusini.

Spishi

Makazi

Spishi zote mbili wamezoea kuishi katika mazingira yabisi kamajangwa au nusu jangwa.

Ngamia nundu-moja anapatikana katikaUarabuni,Mashariki ya Kati hadiPakistani,Afrika ya Kaskazini,Somalia na kaskazini yaKenya. Katikakarne ya 19 walipelekwaAustralia walipozoea haraka; kwa sasa takribani ngamia pori 700,000 wako kule. Spishi hii inavumiliajoto kali lakini piabaridi zausiku kwenyeSahara. Anaweza kubadilishahalijoto yamwili wake kati yasentigredi 34 na 41 kulingana na mazingira.

Ngamia waAsia yuko katika kanda inayoanziaAnatolia hadiManchuriakaskazini mwaChina. Amezoea zaidi baridi yaAsia ya Kati; wakati wa majira barafu halijoto ya mazingira inafikia -30°C. Joto kali inampa matatizo kidogo na kumchelewesha.

Spishi zote mbili zinakutana katika nchi kadhaa, kuanziaUturuki,Uajemi,Afghanistan hadiPakistani.

Mwili

Umbile lao limelingana na mazingira ya jangwani.Miguu ni mipana na kuzuia wasizame chini kwenyemchanga.Nywele ni ndefu, hivyo zinakinga dhidi ya joto na baridi.

Nundu ni mahali pastoo ya akiba yamafuta; kama ngamia anapitia mahali pasipochakula anatumia mafuta kwanishati ya mwilini. Hahitaji kula kwa kipindi hadi siku 30.

Wanaweza kushikalita 100–150 mwilini na kuendelea jangwani bila kunywamaji kwawiki mbili. Penye majani mabichi ya kutosha, na kama joto si kali mno, ngamia anaweza kuendelea bila kunywa kwa wiki kadhaa.

Shingo ni ndefu kwa sababu kwa chakula anapendelea majani ya miti na vichaka.

Maisha

Ngamia wa Asia (C. bactrianus) ana nundu mbili

Ngamia ni wanyama wa kijamii na kwa asili huishi katika makundi yadume mmoja na majike kadhaa. Siku hizi kuna ngamia wa Asia mamia kadhaa kwenye pori ambao ni mabaki ya ngamia pori wa zamani. Wako China naMongolia.

Ngamia nundu-moja si wanyama wa pori asilia tena; inaaminiwa walitokea Uarabuni. Lakini kuna wanyama waliotoroka huko Australia na Amerika wanaoishi peke yao, hawafugwi.

Ngamia na binadamu

Binadamu akiongozana na ngamia

Ngamia wamefugwa nabinadamu tangu miaka 5,000–6,000 iliyopita. Leo hii mifugo hao ni takribanmilioni 19 na idadi kubwa, yaani milioni 14, wako Afrika, milioni 7 pekee nchini Somalia na milioni 3.3 nchiniSudan.

Watu hufuga ngamia kwa kubeba watu na mizigo. Nywele zao ni aina yasufu inayotumiwa kutengenezea mashuka, mahema na pia vitambaa vyanguo. Wanachinjwa kwanyama yao.

Ngamia hukamuliwa pia kamang'ombe. Katika nchi yabisi kiasi chamaziwa yao yanalingana na ya ng'ombe.

Katika miaka ya nyumaWamasai waKenya na piaTanzania wameanza kufuga ngamia baada ya kuona ya kwamba ng'ombe zao walikufa wakati wa ukame lakini ngamia waliendelea kuishi na kutoa maziwa.

Ngamia anachukua chakula chake kwenye mti wenye mizizi mirefu kushinda manyasi yanayoliwa na ng'ombe. Kwa sababu hiyo manyasi hukauka haraka wakati wa ukame kuliko majani ya miti.

Katika Biblia

Katika mazingira ambakoBiblia iliandikwa, ngamia alikuwa mnyama mkubwa kuliko wote wanchi kavu. Ndiyo sababu alitumika katikamethali mbalimbali kwa kusisitiza jambo.

Kwa mfano,Yesu alisema, "Ni rahisi zaidi ngamia kupenyatundu lasindano kulikotajiri kuingiambinguni" (Mk 10:23-27).

Picha

  • Ngamia nundu-moja sokoni huko Nouakchott, Mauritania
    Ngamia nundu-moja sokoni huko Nouakchott,Mauritania
  • Ngamia wakifanya kazi ya msafara
    Ngamia wakifanya kazi ya msafara
  • Ngamia nundu-mbili huko Kirgizia
    Ngamia nundu-mbili hukoKirgizia
  • Mwenyeji wa Turkmenistan akipanda ngamia yake mnamo 1905–1915
    Mwenyeji waTurkmenistan akipanda ngamia yake mnamo 1905–1915
  • Ngamia wawili tayari kwa safari
    Ngamia wawili tayari kwa safari

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Spishi zaArtiodactyla zilizo hai hadi sasa
Himaya:Animalia · Faila:Chordata · Ngeli:Mammalia · Ngeli ya chini:Eutheria · Oda ya juu:Laurasiatheria
NusuodaRuminantia
Antilocapridae
Giraffidae
Moschidae
Tragulidae
Cervidae
Familia hii kubwa iorodheshwa chini
Bovidae
Familia hii kubwa iorodheshwa chini
FamiliaCervidae
Cervinae
Muntiacus
Elaphodus
Dama
Axis
Rucervus
Panolia
Elaphurus
Hyelaphus
Rusa
Cervus
Capreolinae
FamiliaBovidae
Cephalophinae
Hippotraginae
Reduncinae
Aepycerotinae
Peleinae
Alcelaphinae
Pantholopinae
Caprinae
Nusufamilia hii kubwa iorodheshwa chini
Bovinae
Nusufamilia hii kubwa iorodheshwa chini
Antilopinae
Nusufamilia hii kubwa iorodheshwa chini
FamiliaBovidae (nusufamiliaCaprinae)
Ammotragus
Arabitragus
Budorcas
Capra
Capricornis
Hemitragus
Naemorhedus
Nilgiritragus
Oreamnos
Ovibos
Ovis
Pseudois
Rupicapra
FamiliaBovidae (nusufamiliaBovinae)
Boselaphini
Bovini
Strepsicerotini
FamiliaBovidae (nusufamiliaAntilopinae)
Antilopini
Saigini
Neotragini
NusuodaSuina
Suidae
Tayassuidae
NusuodaTylopoda
Cetartiodactyla(Divisheni bila tabaka, juu ya Artiodactyla)

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia:Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ngamia&oldid=1152085"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp