Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

C

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
AaBbCcDd
EeFfGgHhIiJj
KkLlMmNnOoPp
QqRrSsTtUuVv
WwXxYyZz
(Kwa matumizi ya Kiswahili)
chdhghkh
mbmvndngng'nj
nynzshth
Herufi C kwa maandishi mbalimbai
Herufi C kwa maandishi mbalimbai

C ni herufi ya tatu katikaalfabeti ya Kilatini. Katika matumizi yaKiswahili kwa kawaida inatokea tu pamoja na "h" kuwa "ch". C peke yake si kawaida katika maneno ya Kiswahili isipokuwa katika majina ya kigeni.

Maana za C

[hariri |hariri chanzo]

Historia ya herufi "C"

[hariri |hariri chanzo]
Kiebrania
gimel
Kifinisia
gimel
Kigiriki
Gamma
Kiitalia
cha awali: C
Kilatini
C
גPhoenician gimelClassical Greek GammaEarly LatinLate Latin C

Asili ya herufi C ni pamoja na G katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kamaKietruski. Wagiriki walipokea kutokaWafinisia.

Wafinisia walikuwa nagimel iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa yangamia wakitumia alama tu kwa sauti ya "g" na kuiita kwa neno lao kwa ngamia "gimel". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "gamma" bila kujali maana asilia ya "ngamia" ilikuwa sauti tu ya "g".

Waitalia ya kwanza hawakuwa na sauti ya "g" wakatumia alama kwa aina ya "k". Waroma wakaipokea hivyo lakini walikuwa na sauti ya "g" hivyo mwanzoni walitumia "C" kwa sauti zote mbili. Baadaye waliona vema kutofautisha kati ya sauti za "k" na "g" wakaongeza mstari kwenye C kuifanya G. "C" ikabaki kwao kwa kuandika sauti ya "k". Lakini katika lugha ya Kilatini matumizi ya awali bado hukumbkwa katika kifupi cha jina "Gaius" linalofupishwa kwa kuandika "C.".

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=C&oldid=1218124"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp