Bunzi-buibui | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Bunzi-buibui akivuta bui-nyani (Hemipepsis sp.) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 4, jenasi 33 katika Afrika ya Mashariki:
|
Bunzi-buibui ninyigu wafamiliaPompilidae walio nakiuno chembemba na kirefu sana (petiole). Ingawa spishi fulani za bunzi wengine hukamatabuibui, Pompilidae ni familia pekee ambayo spishi zote wanatumia buibui kamachakula chamabuu yao.
Nyigu wa familiaSphecidae na wanusufamiliaEumeninae katika familiaVespidae huitwa bunzi pia.
Bunzi-buibui wana kiuno chembamba na kirefu.Spishi kadhaa ni kubwa kabisa yaoda yaHymenoptera na hufikia zaidi yasm 5. Urefu wa spishi nyingine ni sm 1-2.5.Metatoraksi imeunganishwa kwapronoto namesotoraksi, ili nyigu hao hurukahewani vizuri sana. Juu ya hayo,protoraksi ni imara sana, kwa sababu huchimba namiguu yao ya mbele. Wana miguu mirefu yenyemiiba natibia za nyuma ni ndefu, mara nyingi mpaka kutosha kupitia ncha yafumbatio. Tibia za nyuma huwa na mwiba unaoonekana vizuri kwenye ncha ya nyuma. Takriban spishi zote zinamabawa marefu, lakini spishi chache zinajulikana ambazo zina mabawa mafupi au hazina mabawa. Kwa kawaida bunzi-buibui niweusi aubuluu iliyoiva, mara nyingi wenye mng'ao wametali. Walakini, kuna spishi nyingi zilizorangi kali.
Wapevu wa bunzi-buibui hulambochi yamimea mbalimbali.Maua fulani hutegemea sanauchavushaji na bunzi-buibui, k.m.gugu-maziwaPachycarpus asperifolius (jamaa yamkoe) waAfrika Kusini[1]. Kulingana najenasi na spishi bunzi-buibui hukamata spishi nyingi za buibui kama chakula cha mabuu yao wakifunika karibu familia zote za buibui, pamoja natarantula,bui-nyani,buibui-mbweha,buibui wawindaji nabuibui warukaji, ingawa kila mmoja wa bunzi-buibui hushambulia idadi ndogo tu ya spishi za buibui.
Nyigu wa kike akipata buibui humdunga na kumpoozesha. Kwa kawaida buibui aliyelengwa hawezi kuua nyigu, kwa sababu nyigu anaweza kuruka ili kuzuia miguu nakelisera za buibui, kwa hivyo huyu hupambana vikali ili kutoroka[2]. Bunzi-tarantula hawashambulii wakati tarantula wapevu wako karibu na au ndani yavishimo vyao. Badala ya hiyo nyigu hutafuta madume wapevu ambao wameacha vishimo vyao kutafuta majike kwa kupandana nao. Kwa wazi nyigu kwanza hutumia mabawa yake kupiga hewa juu ya tarantula akimdanganya kufikiria kuwa analengwa na ndege na kwa hivyo tarantula huitika kwa kujikunja ili kuwa mdogo zaidi na kutokuonekana sana, ambayo halafu hufanya tarantula asiweze kujitetea dhidi ya shambulio la nyigu.
Mara tu buibui amepooza, jike hufanya kishimo na hubeba au kuvuta buibui kuelekea hiki au kwenye kishimo kilichofanywa hapo awali[3]. Takriban nyigu hao wote huishi peke yao na kwa hivyo majike hawachimbi vishimo karibu na kila kimoja. Kwa sababu ya saizi kubwa yamwili wamawindo yao, bunzi-tarantula hutengeneza vishimbo karibu na mahali pa shambulio au kutumia kishimo auhandaki la mawindo. Kwa kawaida bunzi-buibui huwapatia kila mmoja wa mabuu yao mawindo /kidusiwa mmoja ambaye lazima iwe mkubwa ili kutosha kutumika kama chanzo cha chakula wakati wote wa ukuaji wa buu. Kwa kawaidayai moja hutagwa juu ya fumbatio ya buibui na kishimo kufungwa ili buu akue bila kuvurugwa navidusia aumatopasi[3]. Nyigu wa kike anaweza sasa kueneza mchanga au kufanya mabadiliko mengine kwa eneo hilo akiacha mahali pa kishimbo hakionekani.
Yai hutoa buu na huyu hula buibui akivunjakiwambo cha nje kwamandibuli yake. Buu akila kidusiwa wake huokoa mpaka mwishoweogani muhimu kama vilemoyo namfumo mkuu wa neva. Kwa kungojea hadi hatua ya mwisho ya ukuaji anahakikisha buibui haitaoza kabla ya buu hajakua kikamilifu[4]. Mabuu wana hatua tano kabla ya kuwabundo. Tofauti kubwa yamofolojia hazibainika kati ya hatua nne za kwanza isipokuwa saizi. Hatua ya mwisho ikikamilishwa mabuu husukakifukofuko chahariri cha kudumu na huibuka kama wapevu baadaye katikamsimu huo huo au kukaa ndani wakati wa msimu wa baridi kulingana na spishi na wakati wamwaka buu awe bundo[5].
Ceropalinae fulani hutaga mayai yao kwenye buibui anayokiakia bado. wakimpoozesha kwa muda mfupi, na baada ya kutoka katika mayai mabuu ya nyigu hujilisha nje kwa kufyonzahemolimfi. Baada ya muda buibui atakufa na kisha buu aliyekomaa atakuwa bundo. Spishi nyingine hutaga mayai kwenye buibui waliopoozeshwa na bunzi-buibui wengine (kleptoparasitism auudusio baada yawizi).
Ukubwa wa kidusiwa anaweza kuathiri kama yai la nyigu litaendelea kuwa dume au jike. Mawindo makubwa mara nyingi hutoa majike[6].Pepsis thisbe wa kusini magharibi mwaMerikani anaonyesha uwiano wa moja kwa moja kati ya urefu wa mwili wa nyigu mpevu na uzito wa buibui kidusiwa,Aphonopelma echina. Kwa sababu saizi ya mpevu waP. thisbe imedhamiriwa na saizi ya kidusiwa aliyepewa na mama yake, marudio ya saizi za vidusiwa kupitia misimu yataamua ubadilifu wa ukubwa baina ya nyigu wapevu[7].
Kuhusu tabia ya kupandana, madume hupata maeneo ya kukaa ili kutafuta majike walio tayari kwa kupandana na wanaopita. Katikautafiti juu ya bunzi-tarantulaHemipepsis ustulata[8], madume wakubwa wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata maeneo ya kukaa na madume walio na eneo kama hili wanaonekana kuongeza nafasi zao za kupandana kwa sababu majike walio tayari huruka kuelekea mahali pa kukaa panaposhikiliwa na madume hao.
{{cite web}}
:More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)