Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Bunge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chumba cha Wawakilishi katika Bunge laAustralia.
Jumba laWestminster ni Bunge laUfalme wa Muungano.

Bunge ni chombo cha kutungasheria na pia ni mmoja wamihimili mitatu inayoundamfumo wautawala kulingana namgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine nimahakama naserikali.

Bunge ni chombo kinachotokana namfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingiduniani kutokaUingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingiBunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.

Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wautawala waMfalme Henri III katikakarne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili,Bunge la Makabwela naBunge la Mabwanyeye.

Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo waWestminster,Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu waserikali bungeni.

Shughuli za bunge husimamiwa nambunge aliyechaguliwa kamamwenyekiti,rais auspika wa bunge.

Kuna aina mbili za bunge:

  • Bunge la "chumba kimoja" ambako wawakilishi wote wa wananchi hukaa na kufanya maazimio pamoja
  • Bunge la "vyumba viwili" ambako kitengo kikubwa zaidi kina kazi ya kutunga sheria na wabunge wake huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katikamajimbo yauchaguzi yanayotakiwa kuwa takriban naidadi ya wapigakura sawa. Kitengo kingine mara nyingi huitwa "senati" au "chumba cha juu" kwa kawaida ni kidogo zaidi, wabunge wake huchaguliwa ama na wawakilishi wamikoa au majimbo au wanateuliwa pia kufuatana na kanuni zakatiba (k.m. kwa shabaha ya kuwakilisha makundi maalumu katikajamii) namadaraka yake kwa kawaida ni madogo lakini inathibitisha au kukataa sheria zilizoamuliwa na bunge la kwanza; lakini hapa kuna tofauti nyingi kati ya nchi na nchi.[1]

Mabunge ya Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Ona pia

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Kamusibunge kamusi bunge.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Stub iconMakala hii kuhusu mambo yasiasa bado nimbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Bunge&oldid=1395222"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp