Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Bulawayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Bulawayo
Mahali pa Bulawayo
"Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Bulawayo, Rhodesia, sasa Zimbabwe, na watu wawili ambao baadaye walitibiwa ugonjwa wa Marburg. Picha hii ilipigwa Februari 2 au 3, 1975, usiku wa pili au wa tatu baada ya mgonjwa wa virusi vya Marburg #1 kufika. kuwasiliana na vekta isiyojulikana."
"Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Bulawayo, Rhodesia, sasa Zimbabwe, na watu wawili ambao baadaye walitibiwa ugonjwa wa Marburg. Picha hii ilipigwa Februari 2 au 3, 1975, usiku wa pili au wa tatu baada ya mgonjwa wa virusi vya Marburg #1 kufika. kuwasiliana na vekta isiyojulikana."

Bulawayo nimji mkubwa wa pili waZimbabwe wenye wakazi 665,940 (sensa ya 2022[1]). Iko kusini-magharibi ya nchi hiyo, katikati yaMatabeleland. Wakazi walio wengi niWandebele.

Jina la mji linatokana na neno laKindebele "Kwabulawayo" yaani "machinjoni".

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Mji wa leo ulijengwa juu ya mabaki ya boma la mfalmeLobengula. Lobengula aliwahi kujenga boma lake la kwanza1871 takriban kilomita 15 kusini ya mji. Mwaka1881 alihamia penye mji wa sasa.

Mwaka 1893 ufalme wa Lobengula ulishambuliwa na jeshi laCecil Rhodes na mfalme aliamua kuchoma boma lake alipoona alishindwa kuzuia maadui. Waingereza walianzisha mji wao juu ya mabaki ya makazi ya awali. 1897 ilipewa cheo cha manisipaa na kuungwa nareli.

Bulawayo ilikuwa mji ambako upinzani dhidi yaukoloni ulianza na baadaye kitovu cha upinzani dhidi ya serikali yaRobert Mugabe.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://www.citypopulation.de/en/zimbabwe/cities/
Mikoa
Wilaya
Kata
Miji mikubwa
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuBulawayo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Bulawayo&oldid=1337501"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp