Bob Dylan alizaliwa katika familia ya Kiyahudi kwa jina la Robert Allen Zimmerman kwenye hospitali ya St Mary's Hospital mjiniDuluth, Minnesota siku ya24 Mei1941[1][2] . Mababu walifika Marekani kutokaMilki ya Urusi wakati wa mwanzo wa karne ya, baada ya kukimbiapogromu dhidi ya Wayahudi katika nchi hiyo.[3] Wazazi wake Abram Zimmerman na Beatrice "Beatty" Stone waliishi Duluth wakahamia baadaye mjini Hibbing. Hapo Robert alipata elimu yake akianza kupiga muziki alipokuwa mwanafunzi wa shule bado.
Mwaka 1959 alihamiaMinneapolis akajiandikisha kwenye somo la sanaa na muziki ingawa hajasoma hali halisi. Badala yake alianza kucheza muziki katika klabu ya "Ten O'Clock Scholar" katika mtaa wa Dinkytown. Wakati ule alianza kutumia jina la Bob (kifupi cha Robert) Dylan kwa sababu alivutwa sana na ayat za mshairiDylan Thomas[4]. Hapa alishawishwa pia na muziki ya Folk yaPete Seeger,The Kingston Trio naWoody Guthrie
Ilhali kama kijana alikuwa alianza muziki ya Rock aliamua kuhamia kwenda Folk kwa sababu hakuridhika na nafasi ya matini kwenye Rock. Mapokeo ya Folk ikampa nafasi ya kusimulia hadithi na shairi kwa muziki. Alisema "Rock'n'roll kwangu haikutosha. Ina mipigo ya kuvutia lakini uimbaji wake si kamili hauwezi kutaja maisha kwa njia halisi. Nikatambua nikiingia katika muziki ya Folk, napata kitu halisi zaidi. Nyimbo zake zinajaa zaidi tamaa, huzuni, furaha, imani, hisia..."[5]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuBob Dylan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
↑"The thing about rock'n'roll is that for me anyway it wasn't enough... There were great catch-phrases and driving pulse rhythms... but the songs weren't serious or didn't reflect life in a realistic way. I knew that when I got into folk music, it was more of a serious type of thing. The songs are filled with more despair, more sadness, more triumph, more faith in the supernatural, much deeper feelings."; taz. Crowe-1985/>