Katikablogu za binafsi,waandishi hutoa mawazo yao kuhusu masuala ibuka katikajamii na kwa njia hii kuanzia mazungumzo katika intaneti. Wasomaji wanaweza kuchangia na kuendeleza katika mawazo haya kwa kupeana maoni yao yanayoweza kukubaliana na yale ya mwenye blogu au hata kutofautiana. Mawazo haya ya wasomaji huwekwa kwa komenti ambazo huwa pale chini ya blogu.
Wanablogu wanaweza kuchocheahisia nzito katika jamii kama zile za uanaharakati ausiasa.
Ili kuwa na blogu yako binafsi, wafaa kuwa unajua kutumia intaneti na pia uwe na jambo la kuwafahamisha watu au kuwafunza ili upate wasomaji. Wafaa pia uwe na mtindo.
Blogu za kampuni huwa na lengo maalumu ya kuwafahamisha wasomaji kuhusu bidhaa mbali mbali za kampuni. Wenye kampuni huzitumia pia kuwafahamisha wateja na wasomaji kuhusu mambo mapya katika kampuni.
Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano,blogu za maandishi,blogu za mkononi,blogu za picha,blogu za sauti, nablogu za video.
Blogu ya mradi waGlobal Voices inaandika muhtasari wamajadiliano nahabari zinazojitokeza katika blogu mbalimbaliduniani, hasa nje yaMarekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katikabara lao.