Alizaliwa hukoClermont-Ferrand, mkoa waAuvergne.
Alipokuwa na umri wa miaka 3 alifiwa na mama, Antoinette Begon. Hapo baba yake, Étienne Pascal (1588 -1651),wakili namwanahisabati, alishughulikia mwenyewe malezi yake.
Mtoto Blaise alionyesha mapema uwezo wake mkubwa katika masomo, hasa yahisabati nafizikia, hata akakaribishwa katika mikutano ya kisayansi iliyoongozwa naMarin Mersenne, aliyekuwa na mawasiliano na wansayansi bora wa wakati huo, kama vileGirard Desargues,Galileo Galilei,Pierre de Fermat,René Descartes naEvangelista Torricelli.
Tangu1639 hadi1647 aliishiRouen, ambapo baba yake alipewa kazi fulani nakardinaliArmand-Jean du Plessis de Richelieu. Huko, mwaka1640, Blaise Pascal alitunga kitabu chake cha kwanza (Essai pour les coniques), na mwaka1644 alitengenwa mashine yake ya kwanzakalkuleta. Tena mwaka1646, pamoja na baba yake na ndugu zake alikumbatiaitikadi kali yadini yaKikristo yaWajanseni.
Kutokana na afya mbaya, mwaka1650, Pascal aliacha masomo ya hisabati mpaka mwaka1653, alipoandikaTraité du triangle arithmétique, alipofafanuapembetatu inayobeba jina lake.
Kisha kunusurika kiajabu katika ajali ya mwaka1654, Pascal aliacha moja kwa moja masomo ya hisabati na fizikia ili kukazaniafalsafa nateolojia. Tangu hapo alijiunga na marafiki waabasia yaPort-Royal, iliyoanzishwa naaskofuJanseni, akashiriki katika mabishano kati ya wafuasi wa askofu huyo mwenye itikadi kali na wanateolojia wachuo kikuu chaSorbone hukoParis.
Miaka1656 na1657, akitumia jina la bandiaLouis de Montalte, alitolea barua zake za kwanza kwa rafiki yake mmojawapo kuhusu mabishano hayo. scritte da un provinciale ad uno dei suoi amici, sulle dispute della Sorbona. Lakini mwaka1660, mfalmeAlois XIV aliagiza ziteketezwe zote.
Lakini, wakati wa kuandika hizo "Barua toka mkoani", Pascal aliwaza kuandika kitabu kirefu zaidi cha kutetea Ukristo, mbali yaUjanseni. Lakini afya yake mbovu ilikuwa imeharibika zaidi, hata akafa tarehe19 Agosti1662, akiwa na miaka 39 tu.
Miniti ya barua zake ilikusanywa na ndugu na marafiki katika kitabu maarufu kwa jina laMawazo, mchanganyiko wa falsafa,maadili na teolojia unaotetea Ukristo.