Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Otto von Bismarck

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaBismarck)
Otto von Bismarck

Otto von Bismarck (1 Aprili181530 Julai1898) alikuwamwanasiasa mashuhuri waUjerumani katikakarne ya 19.

Akiwawaziri mkuu waPrussia alijengaumoja wa Ujerumani katikavita tatu dhidi yaDenmark (1864),Austria (1866) naUfaransa (1870/71).

KamaChansella waDola la Ujerumani aliongozasiasa ya nchi hadi1890 alipoachishwa naKaisarikijanaWilhelm II.

Maisha yake ya awali

[hariri |hariri chanzo]
Bismarck mwaka1836

Jina lake kamili lilikuwa Otto Eduard Leopold von Bismarck-Schönhausen. Alizaliwa katikafamilia ya kitemi wacheo cha chini katikaufalme waPrussia,mama yake alikuwa wa asili ya kiraia.

Alisomasheria nakilimo kwenyechuo kikuu baada ya kumalizaelimu ya sekondari, halafu akajiunga najeshi kwa utumishi wake wa lazima.

Baada yakifo chababa mwaka1845 akachukuautawala wamashamba ya familia yake.

Mwaka1847 akafungandoa na Marie von Thadden akazaa nayewatoto watatu: Marie (1847–1926), Herbert (1849–1904) na Wilhelm (1852–1901).

Mwanasiasa, mbunge na balozi wa Prussia

[hariri |hariri chanzo]
Bismarck-Monument, Hamburg

Wakati wamapinduzi ya kwanza yakidemokrasia katika Ujerumani (1848/49) alijiunga na siasa akawa mtetezi wahaki za mfalme na mpinzani wa wanademokrasia. Akachaguliwa katikaBunge la Prussia.

Mwaka1851 mfalme wa Prussia alimteua kuwa mwakilishi wa Prussia katika halmashauri yaShirikisho la Kijerumani hukoFrankfurt - wakati ule Ujerumani ilikuwashirikisho lisilo na nguvu yamadola 38 yaliyojitegemea. Madola makubwa katika shirikisho hili yalikuwaAustria na Prussia. Bismarck alikuwa pia na vipindi vifupi vya utumishi kamabalozi wa Prussia hukoSt. Petersburg naParis.

Waziri mkuu wa Prussia

[hariri |hariri chanzo]

Mwaka1862 aliteuliwa na mfalmeFriedrich Wilhelm IV kuwa waziri mkuu wa Prussia. Shabaha yake kuu ilikuwa kuongeza uwezo wa nchi. Aliimarisha jeshi la Prussia dhidi ya upinzani wa wabunge wengi. Jeshi hilo lilipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika vita dhidi ya Denmark ya mwaka 1864. Matokeo ya vita yaliongeza mashindano kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele ndani yaShirikisho la Kijerumani.

Matokeo yake yalikuwa vita ya mwaka 1866. Prussia, pamoja na madola kadhaa madogo, ilishinda Austria na jeshi la Shirikisho la Kijerumani. Shirikisho lilivunjika, Prussia ilimeza madola kamaHannover naHesse yaliyokuwa yameshikamana na Austria ikawa dola kabisa ndani ya Ujerumani. Austria ilijiondoa katika siasa ya Kijerumani naidadi kubwa ya madola ya Kijerumani ilijiunga na Prussia katikashirikisho la Ujerumani ya Kaskazini.

Bismarck alilenga sasa kukamilisha kipaumbele cha Prussia katika Ujerumani. Alitumia nafasi ya magongano na Ufaransa juu yauchaguzi wa mfalme mpya waHispania.KaisariNapoleon III wa Ufaransa alitaka Mfaransa achaguliwe lakini Bismarck alimsukuma mgombea Mjerumani. Katika vita ya maneno yakidiplomasia chansella aliweza kumwaibisha mtawala wa Ufaransa. Napoleoni III alitangaza hali ya vita dhidi ya Prussia lakini madola ya Ujerumani ya Kusini, kama falme zaBavaria naWürttemberg, yalijiunga na Prussia.

Bismarck (sare nyeupe) akimtangaza mfalme wa Prussia kuwaKaisari wa Ujerumani Wilhelms I tarehe18 Januari1871 katika jumba la kifalme laVersailles, Ufaransa.

Vita hii ilikuwa mara ya kwanza ya kwamba Wajerumani wote -isipokuwa Austria- walishikamana pamoja tangu muda mrefu sana. Bismarck alitumia nafasi yaushindi wa jeshi la Wajerumani kuwakusanya viongozi wa madola yote ya Ujerumani katika jumba la Kifalme la Ufaransa huko Versailles. Mfalme wa Prussia Friedrich Wilhelm IV alitangazwa kuwaKaisariWilhelm I wa Ujerumani - cheo hiki hakikutumika katika Ujerumani tangu mwaka1806. Dola la Ujerumani liliunganisha madola yote ya Ujerumani ya kale, isipokuwa Austria, chini ya mfalme wa Prussia aliyekuwa sasa pia na cheo cha Kaisari wa Ujerumani.

Bismarck alikuwa mkuu wa serikali kama Chansella wa Ujerumani.

Bismarck akivaa sare ya kijeshi

Bismarck na ukoloni

[hariri |hariri chanzo]

Bismarck alikuwa kiongozi wa Ujerumani wakati nchi zaUlaya ziliendelea kujipatia pande kubwa za dunia kamakoloni. Mwanzoni alipinga makoloni kwa Ujerumani. Alionagharama kubwa za kupata, kujenga na kutetea koloni akaona ya kwamba faida yoyote ya kuwa nazo hailingani na gharama hizo.

Tangumiaka ya 1870 iliongezeka idadi ya watu katika Ujerumani waliodai koloni kwa sababu mbalimbali. Wengine walidai koloni kama ishara ya nchi kubwa na muhimu, wengine walikuwawafanyabiashara waliotafuta ulinzi wamanowari za Kijerumani kwa ajili yabiashara yao dhidi ya wenzao wa mataifa mengine. Bismarck aliona ya kwamba hali ya Ujerumani haitegemei kuwepo kwabendera yake katika pembe za dunia, bali uhusiano na majirani makubwa katika Ulaya hasaUingereza, Ufaransa naUrusi. Tamko maarufu alipotembelewa na mgeni aliyetaka kumhamasisha kuunda koloni katikaAfrika likawa "Ramani yako ya Afrika ni ya kuvutia sana. Lakini ramani yangu ya Afrika iko Ulaya. Ufaransa iko upande wa kushoto, Urusi upande wa kulia, katikati tuko sisi".[1]

Alipenda kuwahamisha Wafaransa kujipatia koloni kwa matumaini ya kwamba watatumia nguvu zao Afrika na kusahau fikra za kulipiza kisasi baada ya kushindwa na Ujerumani katika vita ya 1870/71.

Tangu mwaka1880 Bismarck alitegemeabungenivyama vya kisiasa vilivyotaka kuunda makoloni, hivyo alilegea na polepole kukubali kuanzishwa kwa makoloni kadhaa. Mwanzoni alitoa tu nyaraka za ulinzi kwa makampuni yaliyopatana kukodi maeneo na watawala wa Afrika na waPasifiki.

Baada ya makampuni hayo kushindwa kuendesha maeneo hayo alikubali pia kuingilia moja kwa moja, kwa mfano baada yaKampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki kushindwa katikavita ya Abushiri mwaka1889. Kwa hiyo Ujerumani ikajiunga na mataifa mengine ya Ulaya katika ugawaji wa Afrika kwa sababu za siasa ya ndani.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Volker Ullrichs (Otto von Bismarck, toleo la nne, Rowohlt, Reinbek 1998) uk 101
Bendera ya Dola la Ujerumani Dola la Ujerumani (1871–1918)
Kipindi cha Mapinduzi (1918–1919)
Jamhuri ya Weimar (1919–1933)
Bendera ya Dola la Tatu Ujerumani ya Kinazi (1933–1945)
Bendera ya Ujerumani Ujerumani (tangu 1949)
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Otto_von_Bismarck&oldid=1398071"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp