Kisayansijina hilo linaweza kutumika kwa maana yaHomo sapiens ili kumtofautisha naviumbehai wengine wajenasiHomo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.
Watu wote walioko leo hii nispishi ileile na tofauti zinazoonekana kati yamaumbile yao katika sehemu mbalimbali zadunia ni ndogondogo tu.
Utafiti juu yaDNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepoAfrika walau miaka 300,000 hivi iliyopita.
Kwa namna ya pekee,upimaji waDNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwamama tu, umeonyesha kuwa binadamu wote waliopoduniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 160,000 hivi iliyopita[3].
Halafu upimaji wakromosomu Y, ambayo kilamwanamume anarithi kwababa tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 120,000 hivi iliyopita[4], kidogo tu kabla ya watu kuanza kuenea katikabara laAsia labda kufuatiapwani zaBahari ya Hindi.
Hata hivyo, miaka hii ya mwisho imegundulika katika baadhi ya wanaume wenyeasili yamakabila yaWabangwa naWambo (Camerun,Afrika ya Kati) aina ya kromosomu Y tofauti sana na ile ya wanaume wengine wote waliowahi kupimwa, kiasi cha kukadiria zimetofautiana miaka 350,000 hivi iliyopita.
Vilevile, upimaji waDNA ya mstari kwa jumla umeonyesha uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio waKusini kwa Sahara, wanaasilimia 1-6 yaurithi wakibiolojia kutoka kwa aina nyingine za Homo, hususanHomo neanderthalensis, ile yapango la Denisova na ile iliyorithiwa na baadhi ya watu wavisiwa vya Andaman (India).
Kama hao waliweza kweli kuzaliana naHomo sapiens na kuachauzao uliojiendeleza maana yake walikuwaspishi moja na yeye. Hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko miaka 200,000 iliyofikiriwa kwanza[5].
Kadiri yaBiblia, binadamu ameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:27), mwenyeroho isiyokufa. Hivyo, Mungu amependa kuwasiliana na watu, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katikaurafiki naye na hatimaye tushirikiheri yake.
Ameshirikishwa naye ukuu juu ya viumbe vyote vinavyoonekana. “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshima” (Zab 8:3-5). “Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu” (Yoh 15:15). Amefanya hivyo kwa maneno na matendo yanayoshikamana sana kwa kuwa maneno yanafafanua matendo, nayo matendo yanathibitisha maneno.
Mungu ametufunulia piaukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusumaana na lengo lamaisha yetu. “Mungu hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (1Tim 2:4). “Mungu si mtu, aseme uongo” (Hes 23:19). Yeye hadanganyiki wala hadanganyi.
Kati ya viumbe vinavyoonekana, mtu tu ninafsi, akiwa na uwezo wa kujifahamu, kujitawala, kujitolea na kupendana na wengine. Basi, anapaswa kulinda hadhi hiyo asitawaliwe natamaa za kila aina. Akifanya hivyo anatimiza mpango waMungu juu yake na kupendana naye.
Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la. “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” (Kumb 30:19-20).
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabayamilele. “Kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” (Ufu 12:7-8).
Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusudini namaadili. “Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (Yoh 5:39-40).
Binadamu niumoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, namwili ulioumbwa naye kwa njia yawazazi.Maumbile hayo yanatakiwa kukamilika kwa kupokea na kutimizaupendo wa Mungu aliyesema, “’Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi’. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwa 1:26-27).
Hivyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa naMwanae ili atuokoe, umehuishwa naRoho Mtakatifu atakayeutukuza siku yaufufuo kwa mfano wa Yesu. “Mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye?… Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?” (1Kor 6:13-16,19).
Utotoni anasukumwa tu nahaja zaumbile lake, ambazo ni muhimu kwake na anazilenga bila ya kuhitaji juhudi.
Lakini akikua anaanza kutambuatunu zamaadili nadini, ambazo ni njema, ni muhimu kwa zenyewe na zinamdai azifuate kwa nia imara hadi afikie lengo.
Kwa bidii za kudumu za namna hiyo anamlenga hasa Mungu, wema mkuu.
Anapopitia misukosuko yaujana asikubali kushindwa navionjo wala asikate tamaa, kwa kuwa Mungu amemuumba atawale hata nafsi yake namwili wake.
Mtu wa kwanza kuumbwa na Mungu kadiri ya Biblia alikuwa Adamu, akifuatwa naEvamkewe. Hapo “Mungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana” (Mwa 1:31).
Hata hivyo, baada yadhambi ya asili anadaiwa bidii katika kutekeleza tunu ili wema alionao uzae matunda.
Basi, apanie kukuza wema aliojaliwa ili kesho awe mtu bora kamamzazi,raia, kiongozi wa dini najamii n.k.
Penye nia pana njia hata ya kuelekeautakatifu utakaokamilika katikauzima wa milele.
Binadamu amekabidhiwa na Mungudunia, lakini hasa amekabidhiwa nafsi yake mwenyewe. Itamfaa nini kujua na kutawalaulimwengu, asipojijua na kujitawala kweli?