Katika soka, beki ni mchezaji wa ndani ambayejukumu lake la msingi ni kuzuia wachezaji wa timu pinzani wasifunge katika lango lao, akicheza mbele yaGolikipa.
Kuna aina nne ya mabeki: Beki wa kati, Mfagiaji, Beki wakabaji na Beki wasaidizi. Beki wa kati na Beki wakabaji ni nafasi ambazo ni muhimu katika mifumo mingi. Beki wasaidizi na wafagiaji hutegemea aina ya mfumo unaotumika.
Beki wa kati (kwa jina lingine mlinzi/walinzi wa kati) hulinda eneo lililopo mbele ya lango moja kwa moja, wakiwa uwanjani hujaribu kuwazuia wachezaji wa timu pinzani hasahasa washambuliaji wasifunge. Wanaweza kufanya hivi kwa kuzuia mashuti yapigwayo, kuzuia mipira ya juu kwa kuipiga vichwa na kuwa karibu na mchezaji wa timu pinzani ili kupunguza urahisi wa mchezaji kupigiwa pasi.
Mfumo maarufu wa 4-4-2, beki wa kati wawili hutumika.
Katika mchezo wa kawaida, Beki wa kati wana nafasi ndogo sana ya kufunga. Hata hivyo, wakati wa upigaji wa mipira iliyokufa aidha kona na faulu, beki hupanda katika eneo lapenalti la timu pinzani kwani huwa na uwezo mkubwa wa kuicheza mipira ya juu kwa kichwa. Wakati huo, beki wasaidizi auviungo wa kati huziba nafasi ya beki wa kati kwa muda.
Baadhi ya beki wa kati wanajulikana sana kwa uwezo wao wa kupiga mipira iliyokufa kwa ufasaha zaidi hasa ikiwa katika umbali mrefu kutoka lango la timu pinzani. Beki wa kati waBraziliDavid Luiz,Alex, naNaldo wanajulikana zaidi kwa upigaji wa mipira ya aina hii, upigaji wao ni wa kutumia nguvu zaidi.
Katika mpira wa kisasa, timu nyingi hutumia beki wawili au watatu wa kati wakicheza mbele ya golikipa. Mfumo wa 4–2–3–1, 4–3–3 na 4–4–2 hutumia beki wawili wa kati.
Kuna aina mbili za ukabaji zinzotumiwa na mabekiwa kati, kukaba kwa nafasi, ambapo kila beki huwa na nafasi yake maalumu uwanjani, na kukaba mtu kwa mtu ambapo kila beki humkaba nmshambuliaji maalumu wa timu pinzani.
Mfagiaji (kwa jina linginelibero) ni aina ya beki wa kati mnyumbulifu anayeondoa mipira mshambuliaji akifanikiwa kupita ukuta wa mabeki.[3][4] Nafasi hii ni nyumbulifu zaidi tofauti na aina nyingine ya mabeki ambao hukaba wapinzani kwa karibu zaidi, kwa sababu hioyo, aina hii ya mabeki imepewa jina laKiitalialibero.[5][6]
Japo wafagiaji hutegemewa kujenga mashambulizi ya kushtukiza, jukumu linalohitaji ujuzi mkubwa wa kukokota mipira na kuopiga pasi za ufasaha mkubwa, vipaji vyao mara nyingi havitegemei ujuzi mkubwa wa kukaba. Mfano mfumo wa uchezaji ujulikanao kwa lugha ya kiingereza catenaccio uliotumika zaidi nchiniItalia miaka ya 1960, ulitumia aina hii ya beki ambaye muda mwingi alikuwa akizurura nyuma ya ukuta wa mabeki.[7][8]
Inaaminika kuwa nafasi hii ilishughulikiwa zaidi naFranz Beckenbauer, Gaetano Scirea, na Elías Figueroa, japo sio wa kwanza kucheza katika nafasi hii, wachezaji wa mwanzo wa nafasi hii inawajumuisha wachezaji kama Alexandru Apolzan, Ivano Blason, Velibor Vasović, na Ján Popluhár.[9][10][11][12][13][14][15] Beki wengine wanaoelezewa kama wafagiaji ni pamoja na Bobby Moore, Franco Baresi, Ronald Koeman, Fernando Hierro, Matthias Sammer, na Aldair, kutokana na ufundi wao kwenye kuchezea mpira, uwezo wa kuona na kupiga pasi za umbali mrefu.[9][10][11][16] Japo nafasi hii haitumiki katika mpira wa kisasa, nafasi hii inabaki kuwa ya muhimu sana na yenye kuheshimika.
Beki wa pembeni Caitlin Foord wa timu ya taifa ya wanawake ya Australia katika moja ya michezo ya kombe la alva (2017 Algarve Cup)
Kwa Kiingerezawing-backs ni aina ya walinzi au beki wanaotumika zaidi kushambulia timu pinzani. Aina hii ya mabeki wanaweka nguvu kubwa zaidi kwenye kushambulia zaidi ya kukaba, lazima wawe na uwezo wa kurudi nyuma kuzuia mashambulizi au kupunguza athari za ushambuliaji za timu pinzani. Kazi za mabeki hawa hutofautiana kulingana na aina ya mfumo ya timu, kuna mifumo inayowalazimu kukaba zaidi na mingine inawapa uhuru wa kushambulia zaidi. Mabeki hawa mara nyingi hutumika katika mifumu yenye mabeki watatu wa kati, na mara nyingine huitwa viungo.
Katika mabadiliko ya soka la kisasa, mabeki wasaidizi ni mjumuisho wa viungo wa pembeni na mabeki wakabaji. Hivyo basi, ni eneo linalohitaji matumizi mengi ya nguvu. Mabeki wasaidizi ni nafasi ya kiujumla sana, na mara nyingi hutegemewa kucheza upana kwa timu zisizotumia winga.[17]
↑Damele, Fulvio (1998).Calcio da manuale. Demetra. uk. 104.
↑"La leggenda della Grande Inter" [The legend of the Grande Inter] (kwa Italian). Inter.it. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 19 Oktoba 2012. Iliwekwa mnamo10 Septemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuBeki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.