Barua niujumbe wa kimaandishi unaotumwa kwamtu mwingine au watu wengine. Inawezekana kumwachia mtu ujumbe wa kimaandishi yaani barua mahali fulani lakini mara nyingi barua inatumwa kwa njia ya mtume au shirika linalofanya kazi hiikibiashara.
Kwa kawaida siku hizi barua inaandikwa kwenyekaratasi ama kwakalamu ama kwataipureta ama kwa kutumiakompyuta naprinta. Karatasi ya barua hukunjwa na kuwekwa ndani yabahasha yenyejina naanwani ya mpokeaji juu yake. Siku hizi idadi kubwa ya ujumbe inaandikwa kwa njia yabaruapepe.
Mara nyingi kulikuwa na vituo vya pekee kila baada yakilomita kadhaa ambako watarishi walisubiri kufika kwa barua pamoja nafarasi waliotunzwa katika vituo hivyo. Kwa njia hii Waroma waliweza kusafirisha ujumbe takriban kilomita 80 kilasiku, yaani ilichukua takriban siku 60 kupeleka barua kutoka Roma hadi Misri kwa njianchi kavu (kilomita 3,200). Kamahali ya hewa iliruhusu,usafiri kwajahazi muda huo uliweza kufupishwa kiasi.
Katika miaka 400 iliyopita makampuni ya binafsi na za serikali zimepanua huduma za kusafirisha na kufikisha barua. Kama nitaasisi ya serikali kwa kawaida huitwaposta.
Kuhusugharama, kuna mbinu mbiliː ama mpokeaji analipa gharama za usafirishaji wakati wa kupokea barua, au mwenye kutuma barua analipa gharama wakati wa kutuma. Nchi nyingi huwa na mfumo ambako mwenye kutuma ananunuastempu kwa gharama ya usafirishaji; stempu hizo ni vipande vya karatasi vyenyethamani maalumu ambavyo vinabandikwa kwagundi kwenye bahasha na kugongwamhuri ili zisitumiwe tena.
Katikahistoria ndefu ya matumizi ya barua ilitokea kawaida namna ya kutunga na kuandika barua. Bahasha au sehemu ya nje ya barua huwa na majina ya mpokeaji na pia ya mwandishi pamoja na anwani zao. Barua yenyewe huwa nahabari kuhusutarehe namahali pa kuandikwa, jina ausahihi la mwandishi, jina la mwandikiwa.
Barua zinatofautiana kama ni barua za binafsi ndani yafamilia, kati yamarafiki auwapenzi, kati ya wafanyabiashara auwateja na wauzaji, kati ya ofisi naraia na kadhalika.
Muundo wa barua ya kirafiki umegawanyika katika sehemu sita ambazo ni: Anwani ya mwandishi, Tarehe, Mwanzo wa barua, Kiini cha barua, Mwisho wa barua na Jina la mwandishi.
Barua ni chombo muhimu katikautamaduni wa kila jamii. Zinategemea kuwepo kwa watu wanaojua kusoma na kuandika. Si lazima ya kwamba kila mtu anayetuma barua au kuipokea anajua kuandika au kusoma, maana inawezekana kutumia msaada wa watu wengine. Lakinimawasiliano kwa barua ni uhamasisho mkubwa kwa watu kujifunza na kuboreshaelimu hiyo.