Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Banjul

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jiji la Banjul
NchiGambia
MjiBanjul
WilayaBanjul
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla357 238
Muonekano wa Mji wa Banjul
Mahali pa Banjul katika Gambia
Banjul mjini
Geti yaArch 22 ya kuingia mji wa Banjul

Banjul nimji mkuu waGambia.Mji wenyewe una wakazi 34,828 pekee[1] lakini pamoja na mitaa ya nje ni zaidi yanusumilioni.

Banjul iko kwenyekisiwa cha Mt. Mariamu (au: Kisiwa cha Banjul)mdomoni mwamto Gambia unapoishia katikabahari yaAtlantiki.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Waingereza walianzisha mjimwaka1816BK kama kituo chabiashara na kituo cha kijeshi cha kukomeshabiashara ya watumwa.Jina la mji lilikuwa "Bathurst" kufuatana naHenry Bathurst aliyekuwawaziri wamakoloni wakati ule.

Mwaka1965 Bathurst ilikuwa mji mkuu wa nchi huru ya Gambia. Mwaka1973 jina lilibadilishwa kuwa Banjul.Tarehe22 Julai1994 palikuwa namapinduzi wa kijeshi yaliyoanzishautawala waRaisYahaya Jammeh. Geti la mji "Arch 22" lilijengwa kama kumbukumbu ya mapinduzi haya.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Banjul nikitovu cha utawala na biashara katika Gambia.

Mawasiliano ndani ya nchi ni hasa kwa njia yaferi kwenye mto Gambia hadi mji waBarra.

Msingi wauchumi nikilimo, hasakaranga,nta,mawese nangozi zinasafirishwa kutokabandari ya Banjul.

Banjul inauwanja wa ndege wa kimataifa.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Statoids, Districts of Gambia, (2003), seeBanjul District(Kiingereza)
Wakazi ya Infobox - Statoids, Gambia Divisions, 2003, seeBanjul Division(Kiingereza)

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuBanjul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Banjul&oldid=1210875"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp