Bangladesh (pia:Bangladesh; kwaKibengali: বাংলাদেশ, bāṃlādeś) ni nchi yaAsia ya Kusini. Imepakana naUhindi pande zote barani isipokuwa mpaka mfupi wakm 193 naMyanmar upande wa kusini-mashariki napwani yaGhuba ya Bengali.Ni nchi ya nane kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani na miongoni mwa nchi zenye msongamano mkubwa wa watu na wakazi wanaozidi milioni 170 ndani ya eneo la kilomita za mraba 148,460.Dhaka ndio mji mkuu na jiji kubwa zaidi, ni kituo cha kitaifa cha kisiasa, kifedha na kitamaduni
Mwaka1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini yauongozi waMahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasaumoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenyeitikadi kali wa pande zote mbili.
Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Tarehe 14/15 Agosti1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili zaUhindi na Pakistan.Mgawanyo wa Uhindi ulikuja navita na kumwaga kwadamu nyingi. Bengali yenyewe iligawanyika kwa sababu wakazi wengi wa mashariki walikuwaWaislamu, tofauti na Wabengali wengine waliokuwaWahindu.
Tarehe30 Januari1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitakausawa wa Waislamu na Wahindu.
Wakati ule Bengali ya mashariki ilikuwa nchi moja pamoja naPakistan ya leo, bila kujali umbali mkubwa kati ya pande hizo mbili zilizounganishwa nadini.
Iftekhar Iqbal (2010) The Bengal Delta: Ecology, State and Social Change, 1840–1943, Cambridge Imperial and Post-Colonial Studies, Palgrave Macmillan, Pages: 288,ISBN 0230231837
M. Mufakharul Islam (edited) (2004) Socio-Economic History of Bangladesh: essays in memory of Professor Shafiqur Rahman, 1st Edition, Asiatic Society of Bangladesh,Kigezo:Oclc
M. Mufakharul Islam (2007), Bengal Agriculture 1920–1946: A Quantitative Study, Cambridge South Asian Studies, Cambridge University Press, Pages: 300,ISBN 0521049857
Meghna Guhathakurta & Willem van Schendel (Edited) (2013) The Bangladesh Reader: History, Culture, Politics (The World Readers), Duke University Press Books, Pages: 568,ISBN 0822353040
Sirajul Islam (edited) (1997) History of Bangladesh 1704–1971(Three Volumes: Vol 1: Political History, Vol 2: Economic History Vol 3: Social and Cultural History), 2nd Edition (Revised New Edition), The Asiatic Society of Bangladesh, Pages: 1846,ISBN 9845123376
Sirajul Islam (Chief Editor) (2003) Banglapedia: A National Encyclopedia of Bangladesh.(10 Vols. Set), (written by 1300 scholars & 22 editors) The Asiatic Society of Bangladesh, Pages: 4840,ISBN 9843205855
Srinath Raghavan (2013) ‘1971: A Global History of the Creation of Bangladesh’, Harvard University Press, Pages: 368,ISBN 0674728645
1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuBangladesh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.