Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Bahari ya Sulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Sulu kati ya Borneo na Ufilipino.
Papa anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Twanga ya Tubbataha, Bahari la Sulu, Ufilipino.

Bahari ya Sulu (kwaKifilipino;Dagat ng Sulu; kwaKiingereza: Sulu Sea) ni sehemu yaBahari Pasifiki iliyopo kati yaUfilipino nakaskazinimashariki mwakisiwa cha Borneo (sehemu yaMalaysia), ikipakana upande moja nafunguvisiwa la Sulu (ng'ambo yakeBahari ya Celebes) na kwa upande wakaskazinimashariki na kisiwa chaPalawan (ng'ambo yakeBahari ya Kusini ya China).[1][2]

Jiografia na ekolojia

[hariri |hariri chanzo]

Uso wa sehemu hii yabahari inakilomita za mraba 260,000.Kina chawastani nimita 1139.

Ndani ya Bahari ya Sulu ikoHifadhi ya Taifa ya Tubbataha Reef iliyoorodheshwa naUNESCO kati yaUrithi wa Dunia.[3]

Kusinimagharibi mwa Bahari ya Sulu kunavisiwa ambakokasa wanategamayai yao, hasaKasa Uziwa (chelonia mydas) naKasa Mwamba (eretmochelys imbricata).

Maharamia

[hariri |hariri chanzo]

Bahari ya Sulu inahistoria ndefu yauharamia uliostawi katika mapambano baina yaWahispania (waliotawala sehemu za visiwa vya Ufilipino) na wapinzani waowazalendo.

Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia uharamia ulipata nguvu tena. Mara nyingi ni makundi ya maharamia hadi kumi wanaoshambulia hasamaboti madogo yamizigo na yaabiria pamoja nawavuvi. Katikamiaka ya 1980 takriban mashambulio 100 yalikadiriwa kilamwaka katika Bahari ya Sulu.[4]:60 Maharamia wa eneo hili wanahofiwa kwa sababu wanaua haraka kuliko kawaida na pia wanateka nyara.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Coron Bay, Philippines : UnderwaterAsia.info".www.underwaterasia.info. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 5 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo23 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Sulu Sea, Philippines : UnderwaterAsia.info".www.underwaterasia.info. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 1 Juni 2016. Iliwekwa mnamo23 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. C.Michael Hogan. 2011.Sulu Sea. Encyclopedia of Earth. Eds. P.Saundry & C.J.Cleveland. Washington DC
  4. Liss, Carolin (2011).Oceans of Crime. Maritime Piracy and Transnational Security in Southeast Asia and Bangladesh. Singapore: ISEAS Publishing.ISBN 978-981-4279-46-8.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Bahari ya Aktiki
Bahari ya Atlantiki
Bahari ya Adria ·Bahari ya Aegea ·Bahari ya Åland ·Bahari ya Alboran ·Bahari ya Argentina ·Bahari ya Azov ·Bahari ya Baleari ·Bahari ya Baltiki ·Bahari ya Bothnia ·Bahari ya Eire ·Bahari ya Funguvisiwa ·Bahari ya Greenland ·Bahari ya Hebridi ·Bahari ya Ionia ·Bahari ya Irminger ·Bahari ya Karibi ·Bahari ya Kaskazini ·Bahari ya Kati ·Bahari ya Kiselti ·Bahari ya Krete ·Bahari ya Labrador ·Bahari ya Levanti ·Bahari ya Libya ·Bahari ya Liguria ·Bahari ya Marmara ·Bahari ya Myrto ·Bahari ya Norwei ·Bahari Nyeusi ·Bahari ya Sargasso ·Bahari ya Thrakia ·Bahari ya Tireni ·Bahari ya Wadden ·Beseni la Foxe ·Ghuba ya Biskaya ·Ghuba ya Botnia ·Ghuba ya Boothia ·Ghuba ya Guinea ·Ghuba ya Hudson ·Ghuba ya Maine ·Ghuba ya Meksiko ·Ghuba ya Saint Lawrence ·Ghuba ya Sidra ·Ghuba ya Simba ·Ghuba ya Ufini ·Ghuba ya Venezuela ·Hori ya Baffin ·Hori ya Campeche ·Hori ya Fundy ·Hori ya James ·Mfereji wa Kiingereza
Bahari ya Hindi
Bahari ya Kusini
Bahari ya Pasifiki
Bahari ya Arafura ·Bahari ya Bali ·Bahari ya Banda ·Bahari ya Bering ·Bahari ya Bismarck ·Bahari ya Bohai ·Bahari ya Bohol ·Bahari ya Camotes ·Bahari ya Ceram ·Bahari ya Chile ·Bahari ya China Kusini ·Bahari ya China Mashariki ·Bahari ya Halmahera ·Bahari ya Java ·Bahari ya Koro ·Bahari ya Grau ·Bahari ya Japani ·Bahari ya Matumbawe ·Bahari ya Molucca ·Bahari ya Njano ·Bahari ya Okhotsk ·Bahari ya Salish ·Bahari ya Savu ·Bahari ya Seto ·Bahari ya Shantar ·Bahari ya Sibuyan ·Bahari ya Solomon ·Bahari ya Sulawesi ·Bahari ya Sulu ·Bahari ya Tasmania ·Bahari ya Ufilipino ·Bahari ya Visayan ·Ghuba ya Alaska ·Ghuba ya Anadyr ·Ghuba ya Carpentaria ·Ghuba ya Fonseca ·Ghuba ya Kalifornia ·Ghuba ya Moro ·Ghuba ya Panama ·Ghuba ya Tonkin ·Ghuba ya Uthai
Bahari zisizounganika na nyingine
Nyinginezo
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuBahari ya Sulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Bahari_ya_Sulu&oldid=1429242"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp