Kwa hiyo eneo lote la uso wa bahari hii ni kilomita za mraba 70,560,000 km²; kina cha wastani ni mita 3,741 ilhali kina kikubwa kinafikia mita 7,906. Mjao wake nikilomita za ujazo 264,000,000 km³ inayolingana na asilimia 19.8% ya mjao wa bahari zote duniani.
Kama kawaida, pale ambako mabamba yanaachana kuna nafasi inayoruhusu kupanda juu kwa joto namagma kutokakiini cha dunia na kutokea kwavolkeno pamoja na safu za milima chini ya maji.
Tetemeko la ardhi natsunami ya 2004, iliyosababisha uharibifu na vifo katika sehemu za kaskazini za Bahari Hindi, ilisababishwa na mwendo wa ghafla la bamba la Australia juu ya bamba la Uhindi.
Kwa jumla Bahari Hindi ina halijoto ya juu kulingana na bahari kubwa nyingine za dunia. Tofauti naAtlantiki naPasifiki haina maeneo makubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia hivyo haipokei baridi kutokaAktiki.
Upande wa kazkazini wa ikweta kunamonsuni; upepo kutoka kazkazini-mashariki uko kuanzia Oktoba hadi Aprili, kinyume chake upepo kutoka kusini[1] unaendelea kuanzia Mei hadi Oktoba. Badiliko hili linafuata utaratibu wa kila mwaka na lilikuwa msingi kwa usafiri na biashara katika bahari hii maana iliwezekana kutumia upepo kwa jahazi tangu kale.
Wakati wa badiliko la monsunidhoruba kali zinaweza kutokeas hasa katika Bahari ya Uarabuni na Hori ya Bengali.
Alpers, E. A. (2013).The Indian Ocean in World History. Oxford University Press.ISBN978-0-19-533787-7.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|layurl= ignored (help)
"Oceans: Indian Ocean". CIA – The World Factbook. 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-05-09. Iliwekwa mnamo July 2015.{{cite web}}:Check date values in:|accessdate= (help)
"Limits of Oceans and Seas"(PDF). International Hydrographic Organization, Special Publication N°23. 1953. Iliwekwa mnamo July 2015.{{cite web}}:Check date values in:|accessdate= (help)
"Tuna fisheries and utilization". Food and Agriculture Organization of the United Nations. 2016. Iliwekwa mnamo January 2016.{{cite web}}:Check date values in:|accessdate= (help);Invalid|ref=harv (help) |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.