Eleanor Roosevelt akishika Tangazo kilimwengu la haki za binadamu (1949).
Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu[1] (pia:Tangazo la kilimwengu la haki za binadamu auTaarifa ya Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu[2], kwaKiingereza:Universal Declaration of Human Rights) ni tamko laMkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu yahaki za binadamu lililotolewatarehe10 Desemba1948. Ilikuwa kati ya maazimio ya kwanza kabisa yaUM.
Msingi wahaki hizo uko katika kifungo cha kwanza kinachosema, "Watu wote wamezaliwa huru, wakiwa nahadhi nahaki sawa. Wamejaliwaakili nadhamiri na kupaswa kutendeana kwa roho ya kidugu".
Haki zinaorodheshwa katika vifungu 30 vinavyoeleza haki za msingi ambazo kilamtu anastahili kuwa nazo "bila kubaguana kwarangi,taifa,jinsia,dini,siasa,fikra,asili ya taifa la mtu,mali, kwakizazi au kwa hali nyingine yoyote".
Haki zilizomo katika tangazo hili jinsi zilivyo sisheria ya kimataifa moja kwa moja, lakini zimekubaliwa na kila taifa lililojiunga na UM. Sehemu kubwa ya vipengele vyake imeingia katika mapatano ya kimataifa juu ya haki za kiraia na kisiasa yamwaka1966 na mapatano ya kimataifa juu ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ya mwaka1976 na kwa njia hiyo zimekuwa sehemu ya sheria za kimataifa.
Kwa kuwa kukiri heshima ya asili na haki sawa kwa binadamu wote ndio msingi wa uhuru, haki naamani duniani, Kwa kuwa kutojali na kudharau haki za binadamu kumeletea vitendo vya kishenzi ambavyo vimeharibu dhamiri ya binadamu na kwa sababu taarifa ya ulimwengu ambayo itawafanya binadamu wafurahie uhuru wao wa kusema, kusadiki na wa kutoogopa cho chote imekwisha kutangazwa kwamba ndio hamu kuu ya watu wote, Kwa kuwa ni lazima, ili mtu asishurutizwe kuomba msaada kutokana na maasi ya kupingadhuluma na uonevu, kwamba haki za binadamu ziwe chini yaulinzi wa sheria, Kwa kuwa ni lazima kabisa kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, Kwa kuwa watu wa Umoja wa Mataifa wamethibitisha tena katika Mkataba wao imani yao katika haki za asili, heshima na thamani ya binadamu na katika usawa wa haki kwa wanaume na wanawake, na kwa sababu wamekata shauri la kuendeleza mambo ya starehe na hali bora za maisha ya watu kwa kuwa na uhuru zaidi, Kwa kuwa Nchi zilizo Wanachama zimeahidi, kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, kukuza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wake wa asili, Kwa kuwa kuzitambua haki hizi na uhuru huu ni jambo la maana sana kua kutimiza ahadi hiyo, Kwa hiyo basi, Baraza kuu linatangaza Taarifa hii ya ulimwengu juu ya haki za binadamu kama ndio nguzo ya juhudi kwa watu wa mataifa yote ambayo hatimaye kila mtu na kila jamii ya watu - kwa kushikilia daima Taarifa hiyo - watajitahidi kufundisha jinsi ya kukuza heshima ya haki hizo na uhuru huo. Na mataifa yote yatajitahidi kuzifanya haki hizo zifahamike miongoni mwa Nchi zilizo Wanachama na miongoni mwa watu zinaowatawala.
Kila mtu anastahili kuwa na haki zote za uhuru wote ambao umeelezwa katika taarifa hii bila ubaguzi wowote. Yaani bila kubaguana kwa rangi, taifa, wanaume na wanawake, dini, siasa, fikara, asili ya taifa la mtu, mali, kwa kizazi au kwa hali nyingine yoyote. Juu ya hayo usifanywe ubaguzi kwa kutegemea siasa, utawala au kwa kutegemea uhusiano wa nchi fulani na mataifa mengine au nchi ya asili ya mtu, haidhuru nchi hiyo iwe inayojitawala, ya udhamini, isiyojitawala au inayotawaliwa na nchi nyingine kwa hali na namna yoyote.
Mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za kulindwa. Wote wana haki sawa ya kulindwa kutokana na ubaguzi wowote unaoweza kuvunja taarifa hii na mambo yoyote yanayoweza kuleta ubaguzi huo.
Kila mtu ana haki kamili ya kuhukumiwa vyema hadharani na baraza lililo huru na lisilo na upendeleo katika kutoa uamuzi wa haki zake na wajibu wake na wa makosa yoyote yanayo-mhusu.
Kila mtu anaeshtakiwa kwa kosa la kuvunja sheria ana haki ya kuangaliwa kama si mkosefu mpaka imethibitishwa kisheria, kwa kuhukumiwa hadharani, kwamba ana hatia.
Mtu yeyote asitiwe hatiani kwa tendo lolote au jambo lolote halikupinga sheria ya taifa au ya kati ya mataifa wakati alipotenda. Wala asipewe adhabu kali zaidi kuliko ile iliyokuwamo katika sheria wakati alipofanya kosa.
Kila mtu asiingiliwe bila sheria katika mambo yake ya faragha, ya jamaa yake, ya nyumbani mwake au ya barua zake. Wala asivunjiwe heshima na sifa yake. Kila mmoja ana haki ya kulindaw na sheria kutokana na pingamizi au mambo kama hayo.
Watu wazima, wanaume kwa wanawake wana haki ya kuoana na kuunda jamaa bila ya kizuio chochote kwa sababu ya rangi, taifa na dini. Wana haki sawa ya ndoa wakati wa maisha yao ya ndoa na wakati wa kutenguka ndoa.
Ndoa inaweza kufungwa tu kwa hiari na mapatano kamili kati ya hao wanaotaka kuoana.
Jamaa ni kiungo cha asili cha jamii ya watu, na inastahili kulindwa na watupamoja na serikali.
Kila mtu ana haki ya uhuru wa mawazo, dhamira na dini; haki hii inahusu pia uhuru wa kubadili dini yake au imani, na uhuru wa kubainisha hadharani au faraghani -akiwa peke yake au na watu wengine- dini yake kwa kufundisha kwa vitendo, kuabudu na kwa kuadhimisha.
Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa kushikilia maoni yake bila kuingiliwa kati na uhuru wa kutafuta na kutoa habari na moni kwa njiayoyote bila kujali mipaka.
Kila mmoja anayo haki ya kushiriki katika serikali ya nchi yake yeye mwenyewe binafsi au kwa njia ya mjumbe aliyemchagua kwa hiari.
Kila mmoja anayo haki sawa ya kufanya kazi katika serikali; matakwa hayo huonyeshwa katika uchaguzi halisi unaofanywa muda baada ya muda ambao kila mt hupiga kura na ambao hufanywa kwa kura ya siri na kila mtu hiari yake.
Matakwa ya watu ndio yatakuwa msingi wa utawala wa serikali;hali itajidhihirisha kwenye chaguzi za haki kwa watu wote na ambazo zinafanyika kwa siri au namna nyingine ambayo itahakikisha uchaguzi kuwa huru.
Kila mtu, kama raia, anayo haki ya kutunzwa na anastahili kupata haki zinazotokana na uchumi, starehe na utamadun-ambazo ni lazima kwa hali bora na maendeleo ya nafsi yake-kwa njia ya juhudi ya taifa na ushirikiano kati ya mataifa na kwa mujibu wa utaratibu na utajiri wa kila nchi.
Kila mtu ana haki ya kufanya kazi, ya kuchagua kazi aipendayo, ya kuchagua yenye masharti mazuri na ana haki ya kulindwa asikose kazi.
Kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa na wengine wenye kazi ya namna moja bila ubaguzi.
Kila mfanyakazi anayo haki ya kupata mshahara wa kufaa na unaopendeza utakaomwezesha yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake kuishi katika hali bora, na ahifadhiwe-ikiwa lazimamaisha yake kwa njia nyingine.
Kila mtu anayo haki ya kuunda au kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi kwa ajili ya kulinda haki zake za kazi.
Kila mtu ana haki ya kupumzika na kufanya kazi kwa kiasi cha saa zinazostahili.Pia ana haki ya kupata likizo, kwa kipindi na kupokea mshahara kama vile angekuwa kazini.
Kila mtu anayo haki ya kupata hali bora ya maisha yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake na kupata chakula, mavazi, nyumba, matibabu na hifadhi za lazima kwa maisha yake. Pia ana haki ya kutunzwa wakati wa kazi, wakati wa ugonjwa, wa kutojiweza, ujane, uzee au anapokosa riziki yake kwa kutoweza kujisaidia.
Akina mama na watoto wanastahili kutunzwa na kupewa msaada maalum.Watoto wote-wawe wamezaliwa katika hali ya ndoa ama hapana-lazima watunzwe vyema.
Kila mtu ana haki ya kuelimishwa. Elimu yapasa itolewe bure hasa ile madarasa ya chini. Elimu ya madarasa ya chini ihudhuriwe kwa lazima. Elimu ya ufundi stadi iwe wazi kwa wote. Na elimu ya juu iwe wazi kwa wote kwa kutegemea sifa ya mtu.
Elimu itolewe kwa madhumuni ya kuendeleza barabarahali ya binadamu, na kwa shabaha ya kukuza haki za kibinadamu na uhur wake wa asili. Elimu ni wajibu ikuze hali ya kuelewana, kuvumiliana na urafiki kati ya mataifa na kati ya watu wa rangi na dini mbalilmbali. Kadhalika ni wajibu iendeleze shughuli za Umoja wa Mataifa za kudumisha amani.
Ni haki ya wazazi kuchagua aina ya elimu ya kufunzwa watoto wao.
Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika maisha ya utamaduni ya jamii yoyote, na ana haki ya kufurahia ustadi wa kazi na kushiriki katika maendeleo ya mambo ya sayansi na faida zinazotokana nayo.
Kila mtu ana ya kulindwa kwa kila hali kutokana na mambo ya sayansi aliyoandika, aliyochora au aliyogundua.
Ni haki kila mtu alindwe na taratibu au kanuni za jamii na zinazohusu mataifa mbalimbali ambazo ndani yake uhuru na haki zilizoelezwa katika taarifa hii zinzweza kuhifadhiwa barabara.
Kila mtu ana wajibu kwa watu wa jamii yoyote ambao kati yao tu ndio yanaweza kupatikana maendeleo kamili ya hali ya maisha yake.
Katika kutumia haki na uhuru wake, kila mtu itambidi kufuata kanuni zile tu zilizowekwa na sheria kwa ajili ya kulinda heshima inayotakiwa juu ya haki na uhuru wa watu wengine, na kwa ajli ya kuhifadhi kanuni za haki, usalama na hali njema ya maisha katika jamii ya kidemokrasia.
Uhuru na haki hizi kamwe visitumiwe kinyume cha maazimio na kanuni za umoja wa mataifa.
Hakuna maneno yoyote katika taarifa hii yanayoweza kubashiriwa kwamba yanaruhusu nchi yoyote, kikundi cha watu au mtu fulani kufanya au kushughulika na jambo lolote ambalo nia yake ni kuharibu haki na uhuru zilizoelezwa humu.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuAzimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.