Kwalugha nyingi za dunia jina la "Oceania" (Okeania, Oshania) limekuwa la kawaida kutokana naneno laKigiriki "okeanos" (kwaKilatini: oceanus; kwaKiingereza: ocean). Hivyo "Oceania" yamaanisha "nchi katika bahari". Ila tu hatuoni faida ya kuingiza neno hili katika lugha yaKiswahili kwa sababu ni neno lisiloeleweka vizuri. Mara wataalamu hujadili "Oceania" kuwa visiwa vya Pasifiki pamoja naAustralia; mara wanaona "Oceania" ni visiwa vile pekee bila Australia na wengine wanasema wenyewe "visiwa vya Pasifiki" ingekuwa jina zuri zaidi kama Australia haihesabiwi.
"Australasia" imekuwa jaribio tofauti la kutaja eneo, hasa kati ya wataalamu wa Australia, ila tu halipendwi na watu wengi visiwani. Hivyo imetumiwa zaidi kwa kanda la Australia na visiwa jirani pekee.
Visiwa vyote kwa pamoja (bila Australia yenyewe) hukadiriwa kuwa 7,500 vyenye eneo la nchi kavu lakilomita za mrabamilioni 1.3 vilivyosambaa katika eneo la bahari lakilomita za mraba milioni 70. Takriban visiwa 2,100 vimekaliwa nawatu milioni 14.9.
Visiwa vingi katika Pasifiki nimilima yavolkeno inayoinuka kutokatako la bahari hadi uso wamaji; mara nyingi zinaonyeshakasoko. Visiwa vingine vinajengwa namatumbawe yanayokua juu ya volkeno ambazo zimeishia kidogo chini ya uso wa bahari. Visiwa vingine niatoli ambako matumbawe yamejenga tuta tumbawe kwaumbo lamviringo kuzunguka kisiwa cha kivolkeno.
Sababu ya kutokea kwa volkeno nyingi ni miendo yagandunia katika tabaka zaganda la dunia chini ya bahari.Ngozi ya nje au ganda la dunia hufanywa na vipande mbamlimbali (=mabamba ya gandunia) vinavyoelea juu ya tabaka yamwambamoto nakiowevu. Pale ambako vipande hivi vinagusana mara kwajoto na mwamba moto ulioyeyuka unapanda juu; pale ambao kupanda huku kunatokea haraka tunaona volkeno na hivyo kisiwa kipya kutokea. Mfano ni safu ya visiwa vyaHawaii ambavyo nisafu ya milima ya volkeno inayoanza kwenye tako la bahari, mengine inaonekana kama visiwa, mengine iko chini ya uso wa bahari.
↑Tokelau ni eneo la New Zealand na haina makao makuu kwa jumla kila kisiwa kina chake.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.