Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Augusto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Kaisari Augusto.

Augusto alikuwaKaisari wa kwanza waDola la Roma kuanziamwaka27 KK hadi14BK.Jina lake la kiraia lilikuwaGaius Octavius. AlizaliwaItaliatarehe23 Septemba63 KK.

Octavius alikuwampwa waDiktetaJulius Caesar aliyempendakijana huyo kama baba yake wa kambo na kumteua kamamrithi katikawasia wake.

Historia ya Augusto ina vipindi viwili:

Majina

[hariri |hariri chanzo]
Sanamu ya Kaisari Augusto aliyeabudiwa kama mungu; sadaka zilichomwa mbele yake.

Augusto anajulikana kwa majina mbalimbali.

  • alizaliwa kamaGaius Octavius
  • baada ya kuasiliwa na Caesar alitumia jina lake, hivyo aliitwaGaius Iulius Caesar Octavianus yaani "Julius Caesar wafamilia ya Octavius"
  • tangu mwaka31 KK alitumia piacheo "Imperator" (mwenyeamri, "amiri") kama jina la kwanza
  • mwaka 27 KK alipewa jina la heshima la "Augustus" (anayestahili kuabudiwa) akaitwa "Imperator Caesar Augustus"

Mrithi wa Caesar

[hariri |hariri chanzo]
Kifo cha Caesar (taswira ya 1867) - Tar.15 Machi44 KK Julius Caesar aliuawa naMarcus Junius Brutus naGaius Cassius Longinus.

Alikuwa kijana wa miaka 19 aliyejiandaa kuwaafisa wajeshi kwa mara ya kwanza katikamaisha yake aliposikia habari za kuuawa kwa Julius Caesar. Alikimbilia Roma mara moja alipopata habari ya kuwa Caesar alimsiliki na kumtaja kama mrithi katika wasia. Hapo aliamua kulipiza kisasi juu ya wauaji wa Caesar, hivyo akaingia katikasiasa ya Roma na kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kilichofuata mauaji yakiongozi wa dola.

Kushindana na kupatana na Marcus Antonius

[hariri |hariri chanzo]

Rafiki yakemarehemu,Marcus Antonius, hakukubali wasia akatwaamali yote, lakini watu wengi nawanajeshi wa Caesar walisimama upande wa Octavius. Huyo aliajiriaskari na kujengajeshi na mwaka43 KK alitwaamji wa Roma kwa nguvu ya kijeshi wakati Marcus Antonius alikuwa mbali hukoGallia.

Senati ya Roma ilikubali hatua hii na kumchagua kuwaseneta. Aliendelea kuongoza jeshi la Senati na kumshinda Marcus Antonius kwenye mapigano hukoItalia ya Kaskazini.

Konsuli wa Roma na mtawala katika ushirikiano

[hariri |hariri chanzo]

Baada yaushindi huo alikubaliwa kamakonsuli wa Roma akaendelea kupatana na Marcus Antonius na kujengaushirikiano naye. Pamoja walitawala Roma baada ya kupewa na senatimadaraka ya kidikteta kwa muda wa miaka 5 na baadaye miaka 5 tena.

Mwaka42 KK walifaulu kuwashinda wauaji wa Caesar waliokaaUgiriki na baadaye waligawana eneo ladola kati yao: Octavianus alikuwa mkuu wa sehemu yamagharibi na Marcus Antonius mkuu wa sehemu zamashariki alipomwoaKleopatramalkia waMisri.

Mapigano ya baharini ya Aktium' ya 31 KK' (taswira ya 1672).
Dola la Roma baada ya Augusto.
kijani nyeusi: Majimbo chini ya Roma
kijani nyeupe: maeneo lindwa chini ya Roma yenye kiwango cha kujitawala;
kijani nyeupe nje ya mstari mweusi: Jimbo la Germania Magna lililopotea baada ya mwaka 9

Ushindi juu ya Marcus Antonius

[hariri |hariri chanzo]

Maelewano kati yao yalizorota na mwaka33 KK walitengana. Octavianus alimshinda Marcus katika mapigano yabaharini hukoAktium tarehe2 Septemba31 KK na huyo alijiua pamoja naKleopatra.

Baada ya kuvamia na kutekaMisri Octavianus alirudi Roma mjini mwaka29 KK akawa mtawala pekee.

Raia wa kwanza

[hariri |hariri chanzo]

Huko Roma alishangaza watu wote akirudishamamlaka yake ya kidikteta kwa senati. Aliombwa kuendelea kamamkuu wa jeshi akakubali.

Alikataa kupokea madaraka ya dikteta kwa muda wa maisha yake. Kwa njia hiyo alirudishakatiba yajamhuri iliyotawaliwa na senati na maafisa yake.

Lakini hali halisi alishika mamlaka yote kama mtawala mkuu aliyeheshimutaasisi za jamhuri. Nihekima hii iliyosifiwa na wengi ya kuwa hakuendelea kujipatia cheo chamfalme au cha dikteta akaridhika kuitwaraia wa kwanza.

Utawala wake ulileta kipindi kirefu cha amani ya ndani. Wananchi walioteseka kwa miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe waliweza kujenga maisha upya nauchumi ulistawi.

Milki kubwa ya Misri ilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Hata sehemu nyingi zaGermania ziliingizwa katika dola.

Vita vya pekee vilivyoenda vibaya vilikuwa jaribio la kupanua mipaka ya Roma katikaGermania hadimto Elbe. Wagermania waliangamizalegionitatu nampaka wa Kiroma ulirudishwa hadimto Rhine.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusuKaizari fulani waRoma bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuAugusto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Augusto&oldid=1363272"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp