Katika ramani (Kulia) niasilimia ya Watumwa kati ya wakazi wote katika Bara la Marekani, 1860
Asilimia (kutoka maneno mawili yaKiarabu اصلasl yaani asili, chanzo na مئويةmia 100 ) ni njia ya kutaja uhusiano kati yaidadi mbili tofauti.Alama yake ni%. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ninamba ya 100 ya kiasi kingine.Sehemu yake yamia ni 1 %.
Sasa inawezekana kugawa kiasi kingine kwa ile 1% na kuona inashika asilimia ngapi za kiasi husianifu.
Mfano: Jumla ya maksi kwenyemtihani ni 250.Sheria inasema ya kwamba 65 % ni sharti kwa kupita. Je, maksi ngapi zinahitajika ila kupita mtihani huu?
Jibu: Jumla ni 250, hivyo 250 zachukuliwa kama asilimiamia moja. Sehemu ya mia moja yaani 1 % ni 2.5. Asilimia 65 ni 2.5, zidisha 65 jumla 162.5. Maana yake kuanzia maksi zisizopungua 163mwanafunzi amepita.
Sehemu kamasudusi haifai vizuri kwa sababu asilimia yake ni 16.66 %.
Makala hii kuhusu mambo yahisabati bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuAsilimia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.