Alichangia sehemu kubwa sana katikaelimu yasayansi nafalsafa. mawazo na ugunduzi wake umewachochea watu namaandishi yake yametafsiriwa na kusomwa na watu wengi sana.[1]
Mnamo345 Hermias aliuawa naWajemi na Aristoteli alipokea wito la kuwa mwalimu wa mfalme mteule Aleksander wa Masedonia.
Baada ya Aleksander kuwa mfalme, Aristoteli alirudi Athens 385/334 alipofundishafalsafa yake.
Mnamo323 baada ya kifo cha Aleksander Mkuu alipaswa kuondoka Athens kwa sababu wapinzani wa Masedonia waliongezeka nguvu akahamia Halki alipoagadunia mapema.
Aristoteli alitungakamusi ya falsafa na kitabu juu yaPythagoras na kuna sehemu tu ya maandishi yale yaliyohifadhiwa. Lakini mihtasari aliyotumia kwa masomo ilihifadhiwa ikakusanywa na wahariri wa baadaye na kutolewa kama maandishi yake.
Kati yake kuna maandishi juu yamantiki,fizikia,falaki nametafizikia. Neno "metafizikia" limetokana na Aristoteli kwa sababudhana zake juu ya chanzo na tabia za vitu zilipangwa baada ya maelezo juu ya "fizikia" (hivyo jina "meta-fizikia").
Aristoteli alikusanyaelimu ya wakati wake akajaribu kuipanga katika utaratibu.
Mwenyewe alifundishwa na Plato lakini alitofautiana na mwalimu wake katika mafundisho juu ya tabia za vitu vyenyewe. Plato aliona ya kwamba ujuzi wote tunaopata kupitiamilango ya fahamu hukosa uhakika, si kamili; ujuzi wa kweli unapatikana kwa njia ya roho inayoweza kuelewa kiini cha kitu, wakati milango ya utambuzi inaonaumbo la nje tu. Aristoteli alifikiri tofauti akaona utambuzi kupitia milango yetu ni muhimu zaidi na ujuzi hutegemea utazamaji wa mazingira.
Katika "metafizikia" yake kuna pia dhana juu ya "mwanzilishi" au "mwenye mwendo wa kwanza". Aliona kwamba kila kitu kina mwendo kilichosababishwa na kitu kingine. Hivyomantiki yake ilidai kuwepo kwa chanzo cha mwendo wote akakiita "mwendeshaji asiyeendeshwa" (kwaKigirikiproton kinoun akineton) au kwa lugha nyingine "chanzo asilia". Chanzo asili hiki kwake ni roho au dhana yenyewe (kwa Kigirikinous). Aristoteli aliweza kukiita pia "Mungu".
Kati ya dhana zake za kudumu iko nadharia juu yamichezo tanzia inayotajwa mara nyingi kuhusu maigizo,filamu na hata michezo yakompyuta ya leo. Kufuatana na Aristoteli mchezo tanzia huamshamaono ya watazamaji kama vilependo auchuki,hamu auhofu,furaha auhuzuni nahasira. Ilhali mtazamaji anaingizwa katika hisi hizi roho yake husafishwa wakati wa kutazama mchezo.