Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ario

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea ukimuonyesha Ario chini ya mihuu ya Kaisari Konstantino Mkuu na maaskofu.

Ario (kwaKiberberi:Aryus ; kwaKigiriki Ἄρειος, Areios,250 au256336) alikuwapadri kutokaLibya aliyefanya kazi hukoAlexandria,Misri.[1]

Mafundisho yake[2][3] yalisisitiza kuwaMunguBaba ni mkuu kulikoMwana,[4] akipingaimani katikaUtatu.[5]

Kristolojia yake ilikanushwa na askofu wake,Aleksanda wa Aleksandria, lakini ilienea kotemashariki mwaDola la Roma na kuvurugaKanisa Katoliki kiasi cha kudaiKaisariKonstantino I aitisheMtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka325.

Huomtaguso mkuu wa kwanza, uliokusanya maaskofu wengi hasa wa mashariki, ulikataa hoja zake na kumkiri Mwana kuwa nahali ileile ya Baba.

Hata hivyo vurugu ziliendelea hata kudai ufanyikemtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (383), ambao ni wa pili kati yamitaguso ya kiekumene, nao ukasisitiza na kukamilisha imani ya mtaguso wa kwanza wa Nisea katikaKanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli.

Ingawa imani hiyo ilikubaliwa kura rasmi katika Dola la Roma,Uario ulienea kati yamakabila ya Kijerumani, hasaWagoti naWavandali, hivyo uliendelea hadikarne ya 7 na ya8.

Mpaka leo kunamadhehebu yanayokanusha umungu waYesu Kristo na kusema nikiumbe tu.

Maandishi yake

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Anatolios, Khaled (2011). "2. Development of Trinitarian Doctrine: A Model and Its Application".Retrieving Nicaea. Grand Rapids: BakerAcademic. uk. 44.ISBN 080103132X.Arius, who was born in Libya, was a respected ascetic and presbyter at the church of the Baucalis in Alexandria.
  2. Hanson, R P C (2007).The Search for the Christian Doctrine of God. Grand Rapids: Baker Academic. ku. 127–128.ISBN 0-8010-3146-X.
  3. Kopeck, M R (1985). "Neo Arian Religion: Evidence of the Apostolic Constitutions".Arianism: Historical and Theological Reassessments: 160–162.
  4. Williams, Rowan (2002) [1987].Arius (tol. la Revised). Grand Rapids, Mich: W.B. Eerdmans. uk. 98.ISBN 0-8028-4969-5.
  5. Constantine the Great RulesIlihifadhiwa 21 Novemba 2017 kwenyeWayback Machine. - National Geographic - Retrieved 23 September 2014.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  • Athanasi wa Aleksandria,History of the Arians, London, 2013. limovia.netISBN 978-1-78336-206-6
  • Athanasi wa Aleksandria]].History of the Arians. Online at CCEL.Part IPart IIPart IIIPart IVPart VPart VIPart VIIPart VIII. Accessed 13 December 2009.
  • Artemi, Eirini, The religious policy of the Byzantine emperors since the First to the Fourth ecoumenical council online onhttp://www.impantokratoros.gr/thriskeftikh-politikh.el.aspx
  • Ayres, Lewis.Nicaea and its Legacy: An Approach to Fourth-Century Trinitarian Theology. New York: Oxford University Press, 2004.
  • Hanson, R.P.C.The Search for the Christian Doctrine of God: The Arian Controversy, 318–381. T&T Clark, 1988.
  • Parvis, Sara.Marcellus of Ancyra And the Lost Years of the Arian Controversy 325–345. New York: Oxford University Press, 2006.
  • Rusch, William C.The Trinitarian Controversy. Sources of Early Christian Thought, 1980.ISBN 0-8006-1410-0
  • Schaff, Philip. "Theological Controversies and the Development of Orthodoxy". InHistory of the Christian Church, Vol III, Ch. IX. Online atCCEL. Accessed 13 December 2009.
  • Wace, Henry.A Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D., with an Account of the Principal Sects a.d Heresies. Online atCCEL. Accessed 13 December 2009.
  • Williams, Rowan.Arius: Heresy and Tradition. Revised edition, 2001.ISBN 0-8028-4969-5
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuArio kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ario&oldid=1300256"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp