Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Arigoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaArgoni)


Arigoni
Jina la ElementiArigoni
AlamaAr
Namba atomia18
Mfululizo safuGesi adimu
Uzani atomia39.948
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka83.80K (−189.35°C)
Kiwango cha kuchemka87.30 K (−185.85 °C)
Kiwango utatu83.8058 K
Asilimia zaganda la dunia4 · 10-4 %
Hali maadagesi
Mengineyo{{{mengineyo}}}

Arigoni (pia:argoni, ing.Argon, kut.kigiriki ἀργό(ν) „mvivu“ kwa sababu haipende kumenyuka kikemia) nielementi yenyenamba atomia18 nauzani wa atomi 39.948. Alama yake niAr.

Duniani yapatikana katikaangahewa kama gesi adimu na bwete isiyo na rangi wala ladha. Kwa sababu ya tabia yake ya ubwete kampaundi asilia hazijulikani ila tu zimetengenezwa katika maabara. Katika angahewa ni gesi adimu inayopatikana kwa wingi kwa sababu asilimia moja ya hewa yote ni arigoni.

Inapatikana wakati wa kupoza hewa kwa shabaha ya kupata oksijeni au hidrojeni ya kiowevu.

Kutokanaubwete wake hutumiwa kama gesi ya kuzuia mmenyuko kwa mfano katikavizima moto au ndani yabalbu inapochelewesha kuchomwa kwa nyuzi za balbu.

  • Kipande cha barafu ya arigoni katika tesitubu kikiyeyuka
    Kipande cha barafu ya arigoni katika tesitubu kikiyeyuka
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Arigoni&oldid=1065751"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp